RAIS DKT.SAMIA SULUHU HASSAN AWATUNUKU MAAFISA NA ASKARI NISHANI YA MIAKA 60 YA JWTZ



Rais na Amiri Jeshi Mkuu Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan atunuku Nishani ya miaka 60 ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Ikulu Jijini Dar es Salaam .

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na Majenerali, Maafisa na Askari wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) mara baada ya kuwatunuku Nishani ya miaka 60 kwenye hafla iliyofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 29 Agosti, 2024. 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akimtunuku Nishani ya miaka 60, Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania (CDF) Jenerali Jacob John Mkunda kwenye hafla iliyofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 29 Agosti, 2024. 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Viongozi pamoja na Wageni mbalimbali wakiwa wamesimama wakati Wimbo wa Taifa wa Tanzania na ule wa Afrika Mashariki ukiimbwa kwenye hafla ya kutunuku Nishani ya miaka 60 ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) katika ukumbi wa Jakaya Kikwete, Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 29 Agosti, 2024. 
Baadhi ya Maafisa wa JWTZ waliokidhi  na kuwa  na sifa za  kupata nishani hizo zilizotolewa leo Agosti 29 katika Ukumbi wa Jakaya Kikwete Ikulu Dar  es Salaam. 
(Picha  Zote na   IKULU)

Post a Comment

0 Comments