Na Mwandishi wetu
MADAKTARI ambao bado ni wanafunzi wa Shule ya Mchepuo wa sayansi Chalinze Modern Islamic wametoa hamasa kwa wanafunzi wenzao kupenda masomo ya Sayansi huku lengo likiwa kuzalisha Madaktari wengi nchini.
Wakizungumza na waandishi wa Habari waliofika Shuleni hapo na kujionea upasuaji wa Sungura ambaye upasuaji wake ulikwenda vizuri hali iliyozaa matunda kwa Sungura huyo kubeba mimba na kuzaa watoto sita .
Akizungumza na Waandishi wa Habari Mwalimu wa Taaluma wa Chalinze Islamic Modern Rashidi Hamisi Stambuli leo Julai 12 amesema kuwa anatoa ushauri kwawazazi kutowapangia aina ya masomo ya kusoma ikiwemo fani kutokana na matakwa yao bali kwa kuangalia vipaji walivyo navyo watoto wao na kuwaendeleza kitaaluma.
Daktari Tarajali Mussa Swedi ambaye ni kati ya Madaktari hao wanafunzi katika Shule ya Chalinze Modern Islamic amesema kwa upande wake Sungura aliyemfanyia upasuaji wakati wakisoma mfumo wa hewa amefariki kutokana na waangalizi wake kutofuata masharti kwa sababu alichanganywa na sungura wengine hivyo akataka kumpanda Sungura jike na kwa sababu mshono wake ulikua haujafunga vizuri hali iliyosababisha kifo chake.
"Mimi na Madaktari wenzangu Tarajali tulifuata taratibu zote za upasuaji ila kwa bahati mbaya sungura yule akapoteza maisha ,japo tunajivunia kwa kuona upasuaji wa sungura jike ulienda vizuri ambapo amepona kama jinsimnavyo muona na sasa amezaa watoto sita huku mmoja amefariki kifo cha kawaida nawatano ndiyo hawa mnaowaona"
amesema Mussa mwanafunzi
mwenye njozi za kuja kuwa Daktari wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan.
"Natamani siku moja nije kuwa Daktari wa Mama Samia Suluhu Hassan hata kama atakuwa amestaafu pia natamani siku moja nipate fursa ya kumshika japo mkono wake" amesema Mussa.
Wakati huohuo mwanafunzi Latifa Bakari Njama ameiomba Serikali iwekekipaumbele zaidi katika mtaala wa masomo ya Sayansi hasa kwa kuanzia katika ngazi ya shule ya msingi tofauti na ilivyo sasa huku ikizingatiwa kuongeza wingi wa Madaktari nchini ambao kwa hivi sasa idadi yao haitoshelezi na utoaji wa huduma.
0 Comments