Mkuu wa mkoa Amina Masenza akiwa na viongozi mbalimbali wakikagua moja ya shule ya sekondari na akiuliza kitu kuhusu ujenzi wa shule ya sekondari ya Nyanzwa
Mkuu wa mkoa Amina Masenza akiwa na viongozi mbalimbali wakikagua moja ya shule ya sekondari akielekea kukagua vyoo vya shule ya sekondari ya Nyanzwa
Mkuu wa mkoa Amina Masenza akiwa na viongozi mbalimbali wakikagua vyoo vya shule ya Nyanzwa
Mkuu wa mkoa Amina Masenza akiwa na viongozi mbalimbali wakikagua vyoo katika sekondari ya Ibumu
Na hili ni moja ya jengo ambalo linajengwa kwa ajili ya maabara za shule ya sekondari ya Ibumu
MKUU
wa mkoa wa Iringa Amina Masenza ametoa jumla ya shilingi milioni nne (4,000,000)
kwa ajili ya kuchochea manendeleo ya ujenzi
majengo kwenye shule nne za sekondari ikiwa na lengo la kuhakikisha kuwa wanafunzi
wa shule hizo wanasoma bila kuwa na usumbufu wowote ule.
Akizungumza
wakati wa ziara ya kukagua ujenzi wa shule mpya za sekondari zilizopo tarafa ya
Mazombe mkuu wa mkoa Amina Masenza alisema kuwa serikali ya awamu ya tano chini
ya Rais Dr John Pombe Magufuli imejipanga kuhakikisha wanafunzi wanasoma bila
kulipia kitu mchango wowote ule utakaochangishwa na walimu.
“Mimi
nimetumwa na Rais kusisimamia ila ya chama cha mapinduzi kuhakikisha inatendewa
haki katika kuleta maendeleo hivyo ni lazima nihakikishe wanafunzi wanakwenda
shule na sio vinginevyo maana bila wanafunzi kwenda shule Rais hawezi kunielewa
nitakuwa sijatimiza malengo ya kutoa elimu bila malipo” alisema Masenza
Masenza
alisema kuwa atachangia shilingi milioni moja kwa kila shule za sekondari za
tarafa hiyo ambazo zipo kwenye ujenzi na shule hizo ni Ibumu na Nyanzwa ili
kuhakikisha wanafunzi wanasoma na kuwapunguzia umbali wa kutoka eneo moja
kwenda eneo jingine kuifuata shule.
“Naombeni
tuzikamilishe shule hizi kwa wakati ili kuwapunguzia umbali wa kusoma watoto
wetu haiwezekani wanafunzi hadi kuikuta shule moja ni umbali wa zaidi ya
kilometa kumi na tatu ,jamani hawa ni watoto zetu na maisha yao yanategemea
elimu hivyo ni lazima tuwekeze kwenye elimu” alisema Masenza
Masenza
aliwataka viongozi wa vijiji kuhakikisha kuwa wanafunzi wote waliofulu na
kuchaguliwa kuingia kidato cha kwanza wapelekwe shule kwa wakati na wazazi wote
ambao hawajawapeleke shule watoto wao wachukuliwe hatua kwa kuwa Rais hataki
kuskia kuwa mtoto hajaenda shule.
“Jamani
Rais ameagiza kuwa wanafunzi wote wanatakiwa kuwa shule hata kama hawana sare
za shule sasa huyo mzazi gani ambaye hatakiwa kuwa peleka shule naombeni kabla
sijawakulia hatua nyinyi viongozi basi hakikisheni wanafunzi wote waliofaulu
wanakwenda shule” alisema Masenza
Lakini
mkuu wa mkoa alifanya ziara kwenye shule ya sekondari Kihesa manispaa ya Iringa
na akatoa kiasi cha shilingi laki tano (500,000),shule ya sekondari Ilambilole shilingi milioni moja(1,000,000)
na shule ya msingi Matembo nako alitoa kiasi cha shilingi laki tano (500,000)
pesa zote hizo ni kwa ajili ya ujenzi na ukarabati wa majengo ya shule.
Aidha Masenza alisema
kuwa sasa imefika mwisho kwa watoto wa mkoa wa Iringa kuwa soko la wafanyakazi
wa kazi za ndani wakati wanauwezo wa kuwa viongozi hapo baadae.
“Nasema tena
haiwezekani kila mfanyakazi ukifika daresalaam utasikia katoka Iringa sasa
sitaki kusika swala hilo na wazazi wanaofanya hivyo nitawachulia hatua za
kisheria serikali ya awamu ya tano inataka kuwa na wasomi wengi ili kuasaidia
maendeleo ya nchi”alisema Masenza
Sipia
Kinyowa ni kaimu mtendaji wa kata ya Nyanzwa, Amidu Kilamba diwani wa kata ya
Nyanzwa,Hemerd Wiliamu diwani wa kata ya Ibumu na Justine Mgina mtendaji wa
kata ya Ibumu ni baadhi ya viongozi waliompungeza mkuu wa mkoa kwa ziara
aliyoifanya ya kimaendeleo na kimkatikati kuhakikisha wanafunzi wote wanatakiwa
kufika shule na kusoma bila kubuguziwa na mtu yeyeto.
“Leo
tumefarijiaka sana kuona mkuu wetu kaja na mikakati hasa ya kusaidia kukuza
maendeleo kwenye sekta ya elimu hivyo hatuna budi kumuunda mkono kuhakikisha
kuwa mambo aliyoyaongea tunayafanyia kzi ili kuhikisha wanafunzi wanasoma”
walisema vingozi,
0 Comments