DC KIBAHA ATOA MWEZI MMOJA WAVAMIZI WA MSITU WA DUTUMI KUONDOKA

Mkuu wa Wilaya ya Kibaha, Assumpter Mshama  ametoa mwezi mmoja kwa wavamizi wa eneo la hifadhi ya msitu wa Dutumi kuondoka mara moja ifikapo Oktoba 4 mwaka huu.

DC Assumpter amesema hayo baada ya kwenda kuutembelea msitu huo eneo la Tengefu la hifadhi lililopo katika Mkoa wa Pwani baada ya kupata taarifa kuwa kuna watu ambao wamevamia na wameweka makazi katika eneo hilo isivyo rasmi.

Akizungumza na waandishi wa habari  katika eneo hilo DC Assumpter  amesema kuwa ndani ya msitu huo kuna watu kutoka katika mikoa mbalimbali jumla ya wananchi 3,000 ambao wanaishi ndani ya msitu huo huku wakifanya uharibifu wa kukata miti hovyo na kuichoma kwa lengo la kufanya biashara ya kuchoma mkaa bila ya kuwa na vibali halali kutoka serikalini.
 Mkuu wa Wilaya ya Kibaha, Assumpter Mshama akizungumza na wakazi waliovamia eneo la hifadhi ya msitu wa Dutumi mara baada ya kukagua msitu huo na kukuta uharibifu mkubwa ndani ya Msitu huo.
 Mkuu wa Wilaya Assumpter akimshika mtoto mmoja wapo anayeishi  na wazazi wake kwenye kambi ya watu wanaokata misitu na kuchoma mkaa , hapo alikuwa akiwauliza wazazi hao kuwa hawawatendei haki watoto wao kwani ndani ya kambi hizo hakuna mahitaji muhimu kama hispitali, shule, maji safi  pamoja na malazi yenye hadhi ya kuishi binaadamu
Sehemu ya msitu wa Dutumi ambao umefyekwa miti yote mikubwa na wananchi waliovamia msitu huo


Post a Comment

0 Comments