SERIKALI imekuwa
ikifanya jitihada za dhati katika kukabiliana na changamoto mbalimbali
zinazoikabili sekta ya elimu nchini ikiwa ni pamoja na kuboresha miundombinu ya elimu ikiwemo
ujenzi wa vyumba vya madarasa, Nyumba za walimu, Maabara, Matundu ya vyoo na
mabweni.
Ili kunusuru
kadhia hiyo imeelezwa kuwa moja ya mikakati ni pamoja na wakuu wa Wilaya kuwashirikisha
wananchi pamoja na wadau wa elimu kuchukua hatua madhubuti ili kuboresha
mazingira ya kujifunzia kwa watoto na hatimaye kuwafanya wanafunzi wawe na
furaha na amani.
Hayo yameelezwa na
Katibu Tawala wa Mkoa wa Singida Dkt Angeline Lutambi wakati akihutubia mamia
ya wananchi wa Wilaya ya Ikungi waliojitokeza katika hafla ya uzinduzi wa
Mashindano ya Mpira wa miguu yanayojulikana kama “IKUNGI ELIMU CUP 2017” itakayofanyika katika vijiji vyote 101
vilivyopo katika wilaya ya Ikungi.
Mashindano hayo
yaliyoanza leo Agosti 19, 2017 katika Uwanja wa Shule ya Sekondari Ikungi yanataraji
kufika ukomo siku ya Jumanne Septemba 19, 2017 kwa matazamio ya kuwafikia zaidi
ya wanachi 5000 katika Wilaya hiyo.
Dkt Lutambi
alisema kuwa Mashindano hayo yenye kauli mbiu isemayo “CHANGIA, BORESHA ELIMU
IKUNGI” yamebeba mtazamo chanya wa elimu wenye manufaa kwa wananchi katika
kizazi cha sasa kuelimika na kizazi kijacho.
Alitumia nafasi
hiyo pia kumpongeza Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu huku
akiwaeleza wananchi kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt John
Pombe Magufuli alichagua mtu muhimu kumuwakilisha katika Wilaya hiyo kwani
ubunifu wake katika utendaji una manufaa makubwa kwa wananchi na jamii kwa
ujumla.
Awali akisoma
taarifa ya uzinduzi wa Mashindano hayo, Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji
Jumanne Mtaturu alisema kuwa mashindano hayo ambayo yatakuwa yanalenga
kuhamasisha wananchi na wadau mbalimbali kuchangia vitu mbalimbali kwa ajili ya
kuboresha changamoto zinazoikabili sekta ya elimu katika Wilaya ya Ikungi
ikiwemo upungufu wa nyumba za walimu, maabara ya masomo ya sayansi kwa shule za
sekondari, Madarasa kwa shule za msingi pamoja na vifaa vya kujifunzia.
Sambamba na
mashindano hayo ya mpira wa miguu lakini pia umezinduliwa ufyatuaji wa matofali
kwa ajili ya ujenzi wa maabara ya masomo ya Sayansi ambazo zipo katika hatua za
msingi kwa muda mrefu.
Aidha, zimetolewa
zawadi kwa wanafunzi waliopata daraja la kwanza (Division One) katika matokeo
ya mtihani wa Taifa wa kidato cha sita mwaka huu 2017 na walimu wao ikiwa ni
ahadi iliytolwa na mkuu wa wilaya hiyo.
Mhe Mtaturu
aliahidi kutoa shilingi laki moja kwa kila mwanafunzi atakayepata Daraja la
Kwanza na shilingi milioni moja kwa walimu kwa wanafunzi 10 watakaopata Daraja
la Kwanza.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Singida Dkt Angeline Lutambi akihutubia mamia
ya wananchi wa Wilaya ya Ikungi waliojitokeza katika hafla ya uzinduzi wa
Mashindano ya Mpira wa miguu ya “IKUNGI ELIMU CUP 2017”
Katibu Tawala wa Mkoa wa Singida Dkt Angeline Lutambi akihutubia mamia
ya wananchi wa Wilaya ya Ikungi waliojitokeza katika hafla ya uzinduzi wa
Mashindano ya Mpira wa miguu ya “IKUNGI ELIMU CUP 2017”
Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu akisoma taarifa ya “IKUNGI ELIMU CUP 2017” mbele ya Mgeni rasmi ambaye ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Singida Dkt Angeline Lutambi wakati wa ufunguzi wa mashindano ya mpira wa Miguu.
Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu akibeba tofali lililofyatuliwa na Mgeni rasmi ambaye ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Singida Dkt Angeline Lutambi wakati wa ufunguzi wa mashindano ya mpira wa Miguu ya “IKUNGI ELIMU CUP 2017”
Katibu wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Singida Ndg Jimson Mhagama akibeba tofali lililofyatuliwa wakati wa ufunguzi wa zoezi la ufyatuaji matofali kwa ajili ya ujenzi wa maabara na madarasa.
Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu akifyatua matofali wakati wa ufunguzi wa zoezi la ufyatuaji matofali kwa ajili ya ujenzi wa maabara na madarasa.
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Ikungi akifyatua matofali wakati wa ufunguzi wa zoezi la ufyatuaji matofali kwa ajili ya ujenzi wa maabara na madarasa.
Kikosi cha Timu ya Ikungi United
Kikosi cha Timu ya Puma Combine kilichoshinda goli 3 kwa 2 dhidi ya Ikungi United
Moja ya wanafunzi waliofanya vizuri
katika mtihani wa kidato cha sita kwa kupata Daraja la kwanza akipokea
shilingi 100,000 ikiwa ni ahadi ya Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji
J. Mtaturu
Matofali ambayo yamefyatuliwa na wadau wakati wa ufunguzi wa ufyatuaji
matofali Wilayani Ikungi
Mipira iliyotolewa kwa jili ya timu zote
washiriki wa “Ikungi Elimu Cup 2017”
0 Comments