Wadau mbalimbali wa Baraza la Biashara la Wilaya ya Ubungo, wakimsikiliza MKUU wa Wilaya ya Ubungo Mhe Kisare Makori Leo June 30, 2017 wakati wa ufunguzi wa Baraza la Biashara la Wilaya ya Ubungo
Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo akizungumza kwenye mkutano wa wadau wa Baraza la Biashara la Wilaya ya Ubungo, Leo June 30, 2017 Katibu Tawala wa Wilaya ya Ubungo Ndg James Mkumbo akimsikiliza MKUU wa Wilaya ya Ubungo Jijini Dar es salaam Mhe Kisare Makori wakati akizungumza kwenye mkutano wa wadau wa Baraza la Biashara la Wilaya ya Ubungo, Leo June 30, 2017
Mwenyekiti wa TCCIA-Ubungo Ndg Clement Bocco akisikiliza hoja za wajumbe kwenye mkutano wa wadau wa Baraza la Biashara la Wilaya ya Ubungo, Leo June 30, 2017
MKUU wa Wilaya ya Ubungo Jijini Dar es salaam Mhe Kisare Makori (Kushoto) akiteta jambo na Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg john Lipesi Kayombo wakati mkutano wa wadau wa Baraza la Biashara la Wilaya ya Ubungo, Leo June 30, 2017
Mwanasheria wa Manispaa ya Ubungo Ndg Merick Luvinga akifatilia mkutano wa wadau wa Baraza la Biashara la Wilaya ya Ubungo, Leo June 30, 2017
MKUU wa Wilaya ya Ubungo Jijini Dar es salaam Mhe Kisare Makori (Katikati) akizungumza wakati wa mkutano wa wadau wa Baraza la Biashara la Wilaya ya Ubungo, Kulia ni Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg john Lipesi Kayombo na Mwingine ni Mwenyekiti wa TCCIA-Ubungo Ndg Clement Bocco, Leo June 30, 2017
Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo akimsikiliza kwa makini MKUU wa Wilaya ya Ubungo Jijini Dar es salaam Mhe Kisare Makori kwenye mkutano wa wadau wa Baraza la Biashara la Wilaya ya Ubungo, Leo June 30, 2017
Kushoto ni Afisa Utumishi Mkuu Manispaa ya Ubungo Ndg Ally Juma Ally, Mwingine ni Mchumi Mkuu Manispaa ya Ubungo Ndg Yamo Wambura wakimfatilia kwa makini MKUU wa Wilaya ya Ubungo Jijini Dar es salaam Mhe Kisare Makori kwenye mkutano wa wadau wa Baraza la Biashara la Wilaya ya Ubungo, Leo June 30, 2017
Na Mathias Canal, Dar es salaam
MKUU wa Wilaya ya Ubungo Jijini Dar es salaam Mhe Kisare Makori leo June 30, 2017 amezindua Baraza la Biashara la Wilaya ya Ubungo.
Akihutubiwa wadau mbalimbali waliojitokeza kwenye Mkutano huo wa ufunguzi wa Baraza hilo uliofanyika katika Ukumbi wa Manispaa ya Ubungo uliopo Kibamba CCM, Mhe Makori alisema kuwa lengo la kuanzishwa kwa Baraza la Biashara la Taifa ni uwezeshaji wa wananchi kiuchumi na serikali kwa kushirikisha wadau mbalimbali.
Katika uzinduzi wa Baraza la Biashara Wilaya ya Ubungo Wadau mbalimbali wameshiriki kutoka Sekta binafsi, Mashirika yasiyo ya kiserikali na watu binafsi kutumia fursa zilizopo katika mazingira yanayowazungumza kwa kuwezeshwa kiuchumi.
Mhe Makori alisema kuwa kupitia Mabaraza ya Wilaya wananchi wataongeza uwezo wao wa ubunifu na uzalishaji na biashara ambapo kwa uwezeshaji huo wananchi watafikia matarajio yao ya kuwa na maisha bora.
Alisema kuwa ili kufikia lengo hilo sera mbalimbali zimetekelezwa ikiwa ni pamoja na kupitishwa kwa sera na sheria namba 16 ya uwezeshaji wananchi kiuchumi ya mwaka 2004, Kuundwa kwa baraza la Taifa la uwezeshaji kiuchumi mwaka 2015 na Uanzishwaji na uimarishwaji wa mifuko mbalimbali ya kuwezesha wananchi kiuchumi.
Alisema kuwa kutokana na upya wa Wilaya ya Ubungo ilitakiwa kuunda Baraza lake la Biashara likiwa chini ya Baraza la Mkoa na Taifa.
Mhe Kisare alisema kuwa Kuanzishwa kwa Mabaraza ya biashara ya Wilaya ni kuwa chombo cha mwanzo wa majadiliano kati ya sekta ya umma na sekta binafsi kwa lengo la kuboresha mazingira ya biashara na uwekezaji, Kuwa chombo cha kuratibu, kufuatilia na kutathimini utekelezaji wa Programu mbalimbali za maendeleo ya wananchi kiuchumi.
Kuanzishwa kwa mabaraza ya biashara Wilaya itakuwa ni sehemu ya kupeleka mafanikio ya ukuaji uchumi mpana katika ngazi ya chini ya uchumi wa jamii kwa kuwahusisha wananchi katika majadiliano ya kuibua fursa za uwekezaji kwa ajili ya kuzalisha ajira, kukuza kipato, kuongeza tija na kupunguza umasikini kuanzia ngazi ya Kijiji hadi Wilaya.
Awali akizungumza kabla ya Kufunguliwa kwa Baraza hilo Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo alisema kuwa Baraza la Biashara la Wilaya lina wajumbe arobaini kutoka sekta binafsi na ya Umma, kila sekta ikiwa na wajumbe ishirini kutokana na nyadhifa, nafasi na ujuzi.
Kayombo aliongeza kuwa Baadhi ya wajumbe wanapangwa kwenye kamati/vikundi kazi kwa kuzingatia maeneo ya kipaombele yanayopaswa kufanyiwa kazi.
Mkurugenzi Kayombo alisema kuwa Uzinduzi wa kuanzishwa kwa Baraza hilo ni utekelezaji wa agizo la kuanzishwa mabaraza ya Biashara ya Wilaya lililotolewa na Mwenyekiti wa Baraza la Biashara la Taifa Mhe Jakaya Mrisho Kikwete katika Mkutano wa tano wa Baraza hilo Disemba 4, 2008 uliofanyika Jijini Dar es salaam ambapo alisisitiza uundwaji huo kusimamiwa na Mabaraza ya Mikoa na Taifa.
IMETOLEWA NA;
KITENGO CHA HABARI NA UHUSIANO
HALMASHAURI YA MANISPAA YA UBUNGO.
0 Comments