TRA YAMZUNGUMZIA MSANII DIAMOND PLATINUMZ KUHUSU KODI


 Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipa Kodi kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania, (TRA),  Richard Kayombo (katikati), akitoa hotuba ya ufunguzi wa  semina ya siku moja ya ujasiriamali na elimu ya kulipa kodi kwa waandishi wa habari kwenye ukumbi wa Benki Kuu ya Tanzania jijini Dar es Salaam leo Mei 13, 2017. Kulia ni Mwenyekiti wa semina hiyo, Bi. Angella Msangi na kushoto ni Afisa Kodi Mkuu wa TRA, Bw.Mwangosi
 Waandishi wa habari wakifuatilia hotuba ya ufunguzi

MKURUGENZI wa Huduma na Elimu kwa Mlipa Kodi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bw. Richard Kayombo, ameendelea kukanusha kwamba, Mamlaka hiyo haijamkadiria msanii wa muziki wa kizazi kipya, Diamond Platnamuz kulipa kodi ya shilingi Milioni 400.

Hayo ameyasema leo Mei 13, 2017 wakati akifafanua hoja mbalimbali kwa waandishi wa habari wanaoshiriki semina ya siku moja iliyoandaliwa na TRA ili kutoa elimu ya ulipajin kodi kwa waaandishi na kufanyika kwenye ukumbi wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), jijini Dar es Salaam.

“Tuko kwenye hatua za awali za mazungumzo bado hatujakadiria kodi amnayopaswa kulipa Diamond, na kwa bahatio nzuri tumekaa naye na bado tuko kwenye mazungumzo na sio kweli kwamba tumemkadiria shilingi Milioni 400,” Alisema na kuongeza

“Tunajaribu kujua vyanzo vyake vya mapato, lakini hata kama imetokea mtu umekadiriwa kulipa kodi kwa kiasi Fulani na hujaridhika unayo nafasi ya kukata rufaa kwa Kamishna Mkuu wa TRA, na ndapo hujaridhika na rufaa hiyo ipo Mamlaka nhyingine ambayo iko nje ya TRA, Tax Tribunal, na bodi ya Rufaa za kodi.” Alifafanua Kayombo.

“Hivyo mtu asiwe mnyonge anayo nafasi ya kukata rufaa, tatu ndani ya TRA, na mbili nje ya TRA ikiwa ni pamoja na Mahakamani, kwa hivyo watu wasiogope. Alisema. Awali akifungua semina hiyo.

Bw. Kayombo aliwaasa waandishi wa habari kujenga uzalendo kwa kuunga mkono juhudi za Mamlaka ya Mapato Tanania TRA, katika kuelimisha umma umuhimu wa kulipa kodi ili kuiwezesha serikali kutoa huduma stahiki kwa wananchi.

Hayo yamesemwa leo Mei 13, 2017 na Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipa Kodi kutoka TRA, Bw. Richard Kayombo(pichani juu), wakati wa ufunguziwa semina ya siku moja ya ujasiriamali na elimu ya kulipa kodi kwa waandishi wa habari kwenye ukumbin wa Benki Kuu ya Tanzania jijini Dar es Salaam.

“Najua kihistoria linapokuja swala la kulipa kodi huwa kuna changamoto nyingi watu kuelewa swala hili, lakini napenda niwaeleze ndugu zangu, ili kuiwezesha serikali kutoa huduma stahiki kwa wananchi ni lazima watu walipe kodi, hivyo waandishi wa habari mnao wajibu mkubwa kutumia taaluma yenu kuelimisha umma umuhimu wa kulipa kodi, Alisema  Kayombo.

Bwana Kayombo amesema, TRA kwa niaba ya serikali ya ndiyo chom,bo chenye mamlaka ya kukusanya kodi za serikali katika kutoka kwa watu binafsi, makampuni na taasisi za umma.

“Huduma za usafiri, elimu, afya na miundombinu itakuwa bora tu endapo wananchi watatimiza wajibu wao wa kulipa kodi.” Alisema na kuongeza katika semina hii waandishi wa habari watapata fursa ya kujifunza mambo mbalimbali yahusuyo kodi ikiwemo kodi ya majengo kutoka kwa watalamu wa kodi wa TRA.
  Waandishi wa habari wakifuatilia hotuba ya ufunguzi
  Waandishi wa habari wakifuatilia hotuba ya ufunguzi
 Waandishi wa habari wakifuatilia
 Afisa Mawasiliano Mwandamizi wa TRA, Bi. Rachael Mkundai, (kulia), akiwakaribisha waandioshi wa habatri kwenye semina. Kushoto ni Mwenyekiti wa semina, Bi. Angella Msangi
Bw. Sydney Mkamba, Afisa Kodi Mkuu
Afisa Kodi Mkuu wa TRA, Bw.Gabriel Mwangosi.
 Bw. Emmanuel Herman, kutoka Mwananchi
 Mwenyekiti wa semina akifuatilia
 Bw. Obeid Mwangasa
 Othman Michuzi(kushoto) wa Mtaa kwa Mtaa Blog na Bw. Mushi wa The Habari.com
Anna Nkinda(kulia) kutoka JKCI, na Mhariri wa Habari TBC, Anna Kwambaza.

Post a Comment

0 Comments