Mkurugenzi
wa Taasisi ya Kimataifa ya Kupambana na Trakoma (ITI) akizungumza na washiriki
wa mkutano wa
pili wa mwaka wa nchi 7 za Afrika Mashariki zilizo katika mapambano dhidi ya
ugonjwa wa Trakoma kuhusu uendelezaji wa juhudi za
kuwaelimisha wananchi na kutoa tiba katika maeneo yanakabiliwa na ugonjwa Trakoma kwa nchi
washiriki wa mkutano huo kutoka Kenya, Tanzania, Uganda, Ethiopia, Eritrea,
Sudani na Sudani Kusini.
Mratibu wa Taifa wa
Magonjwa yasiyopewa kipaumbele kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya
Jamii,Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Upendo John Mwingira akiwasilisha
kuhusu mkakati wa kukabiliana na Trakoma kwa kuyafikia maeneo yasiyofikika
kirahisi ya jamii za wafugaji nchini Tanzania wakati Mkutano wa pili wa mwaka wa nchi 7
za Afrika Mashariki zilizo katika mapambano dhidi ya ugonjwa huo unaofanyika
jijini Arusha. Wananchi kutoka Jamii za wafugaji kutoka nchi washiriki
wa mkutano huo bado wanakabiliwa na changamoto ya
ugonjwa wa Trakoma.
Mganga
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Dkt. Frida Mokiti akichangia wakati wa mkutano wa pili wa mwaka wa nchi 7 za
Afrika Mashariki zilizo katika mapambano dhidi ya ugonjwa wa Trakoma jijini
Arusha.
0 Comments