Meneja Ukuzaji Biashara wa Twiga Cement, jamal Yahya akiongea na Revocatus Mwombeki (32) ambye ni mkazi wa Jiji la Mwanza aliyeibuka kuwa mshindi wa kwanza katika droo ya mwisho ya Jijenge na Twiga Cement Afisa msimamizi wa michezo ya kubahatisha Tanzania, Abdallah Hamed(wa pili kutoka kushoto) akifuatilia kwa makini huo katika droo hiyo.( Picha na Adroph Geofrey).
Mkuu wa Masoko na Huduma kwa Wateja wa kampuni hiyo, Martha Haule akiongea na Salum Ismail mkazi wa Mkambalani Mkoani Morogoro ambaye ameibuka mshindi wa tatu na kujinyakulia mifuko 200 ya Cement.
Mkurugenzi wa Masoko, Simon Delens(wa pili kutoka kulia) akiwa kwenye picha ya pamoja na washindi wa wiki iliyopita
Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
DROO ya mwisho ya Jijenge na Twiga Cement imefanyika leo huku mshindi wa mwisho huku mkazi wa Jiji la Mwanza Revocatus Mwombeki (32) akiibuka kuwa mshindi wa kwanza .
Kutokana na ushindi huo Mwombeki ameshinda mifuko 600 ya Twiga Cement Extra ambaye ameshinda bada ya kucheza kwenye droo hiyo iliyoendeshwa kwa majuma manne.
Katika droo hiyo nafasi ya pili ilikwenda kwa Sweya Bulaga (32) aliyepata zawadi ya mifuko 400 ya Cement huku nafasi ya nne ikichukuliwa na Salum Ismail mkaazi wa Mkambalani Mkoani Morogoro ambaye amepata mifuko 200 ya Cement.
Wakati huohuo Hamza Juma (29) Mkaazi wa Nkuhungu mkoani Dodoma aliibuka mshindi na kupata zawadi ya mashine ya kisasa ya kufyatulia matofali kutoka Kiwanda cha Twiga Cement.
Aidha washindi watatu katika droo hiyo waliopatikana wiki iliyopita wamekabidhiwa vyeti vyao vya ushindi ambao ni mshindi wa kwanza Maria Kalinga (35) kutoka Iringa amepata mifuko 600,
Cassian Mihoza amejinyakulia mifuko 400 ya Cement , mkaazi wa Kunduchi Jijini Dar es Salaam na Kennedy Owili mkazi wa Jijini Mwanza ambaye amepata mifuko 200 ya Cement.
Washindi hao wamepatikana katika droo iliyochezeshwa katika Kiwanda hicho cha Twiga Cement kilichopo Wazo Hill Jijini Dar es Salaam.
Akizungumza kwenye mkutano na waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam Ofisa Masoko Simon Delens amewashukuru wananchi wote ambao walijitokeza katika kucheza droo hiyo ambayo ilionekana kuwavutia wengi huku akisema kwamba Twiga Cement inawaandalia mambo mazuri zaidi wateja wake huku akisisitiza kuwa mambo mengi mazuri yatakuja ikiwa ni lengo la kuwafurahisha na kuwavutia wateja.
0 Comments