WATEJA WA TWIGA CEMENT SASA KUNUNUA KWA MPESA





 Afisa Mkuu Biashara wa Vodacom Tanzania, Gregory Verbond (kulia) na Mkurugenzi  Kiwanda cha Saruji cha Simba Cement cha Tanga (TTCL), Reinhardt Swart (kushoto) wakiwekea makubaliano ya mteja  kunua saruji kwa M PESA bila tozo yoyote  popote nchini.

  Afisa Mkuu Biashara wa Vodacom Tanzania, Gregory Verbond (kulia) na Mkurugenzi kiwanda cha Saruji cha Simba Cement Tanga (TTCL), Reinhardt (kushoto) wakibadilishana nyaraka za makubaliano ya mteja kununua Saruji kwa M PESA bila tozo yoyote popote nchini.



 Afisa Mkuu Biashara wa Vodacom Tanzania, Gregory Verbond (kulia) akizungumza mara baada makubaliano na kiwanda cha Saruji cha Simba Cement kwa mteja kununua  Saruji kwa   M PESA bila tozo popote nchini.






 Mmoja wa wakala wa Simba Cement Tanga, Athuman Ali (kulia) alievaa kibagalashia akiwa mmoja wa watu waliohudhuria makubaliano ya utiaji saini wa Ununuaji wa Saruji kwa M PESA baina ya Kampuni ya Vodacom Tanzania na Kiwanda cha Saruji cha Simba Cement cha Tanga leo.
 William Mgazija wa ITV aliesimama nyuma na kushika MIC ni miongoni mwa wahudhuriaji wa makubaliano ya utilianaji wa saini wa manunuzi ya Saruji kwa M PESSA
Waandishi wa habari nao walikuwa miongoni mwa waalikwa wa ushuhudiaji wa utilianaji saini makubaliano ya ununuzi wa Saruji kwa M PESA. Kutoka kushoto alievaa Ushungi ni Amina Omari wa Gazeti la Mtanzania , Betha Mwambellah wa TBC na Maryam Mwandishi wa Jambo leo

KIWANDA Cha Saruji cha Simba Cement (TCCL) cha Tanga, kimeinmgia makubaliano na Kampuni ya simu ya mkononi ya Vodacom Tanzania Limited, kwa mteja kununua saruji kwa kutumia M PESA bila tozo yoyote.
Makubaliano hayo yaliyofanyika leo viwanja vya Hotel ya Tanga Beach na kushuhudiwa na viongozi wa pande zote mbili na kutajwa kuwa yatakuwa mkombozi kwa mwananchi wa kipato cha chini kwa kununua Saruji kwa simu badala ya kutumia Taasisi za pesa na kupanga foleni.
Akizungumza na waandishi wa habari, Afisa Mkuu Biashara wa Vodacom Tanzania, Gregory Verbond, alisema kampuni yake imechukua uamuzi huo wa makubaliano na kampuni ya Cement kwa lengo la kumsaidia mwananchi wa kipato cha chini.
Alisema mteja ataweza kununua Saruji (Simba Cement)  kwa kutumia M PESA na hakutakuwa na tofati ya mnunuzi wa mifuko mingi na michache ambapo hatotozwa ada yoyote mnunuaji.
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa kiwanda cha Saruji, Simba Cement, Renhardt Swart, alisema makubaliano hayo ni moja ya sera za kiwanda kumsaidia mwananchi wa chini kuweza kukabiliana na changamoto za maisha.
Alisema Kiwanda cha Simba Cement daima kiko kwa ajili ya wananchi na faida inayopata inairejesha kwa wananchi na kuwataka kuitumia fursa hiyo ambayo iko na unafuu kwa ununuaji.
Habari kwa Hisani ya Tanga Kumekucha Blog

Post a Comment

0 Comments