MCHEZO WA NGUMI ZA KULIPWA WATAKA MALEZI BORA YA MCHEZO UHO


 Mdau  wa mchezo wa ngumi nchini Chaurembo Palasa akifafanua jambo wakati wa mkutano wa wadau wa mchezo wa masumbwi nchini   kushoto ni Chuku Dusso Ally Bakari na Yassin Abdallah Picha na SUPER BOXING NEWS           
 BAADHI YA WADAU WALIOJITOKEZA KATIKA MKUTANDO WA KUNUSURU MCHEZO WA NGUMI PAMOJA NA MWENENDO WAKE MZIMA KUTOKA KULIA WALIO SIMAMA NI sHOMARI kIMBAU,SHABANI KAONEKA,CHUKU DUSO Mkali Kaizum CHAUREMBO PALAS NA WALIOKAA KUTOKA KUSHOTO NI FIDEL HYNES  ALLY BAKARI NA RATIBU WA MKUTANO UHO SADICK KINYOGOLI
Mdau wa mchezo wa masumbwi nchini Yasin Abdallah katikati akiongea katika mkutano wa wadau wa mchezo wa masumbwi nchini kushoto ni Chuku Duso na kulia ni Chaulembo Palasa Picha na SUPER BOXING NEWS
Katika miaka ya hivi karibuni takwimu zinaonesha kuwa masumbwi ndio mchezo wenye kuingiza pesa nyingi kuliko mchezo wowote duniani, ambapo kwa hivi sasa kinara wa utajiri kupitia mchezo huo ni bondia Floyd Mayweather.
Mkali huyo anafuatiwa na Manny Paquaio ambao wote ni mabondia wanaoshikilia nafasi mbili za juu za utajiri michezoni, huku  michezo mingine ikifuata.

lakini kwa hapa kwetu Tanzania kumekuwa na kilio cha kawaida sana kwa wapenzi na washabiki wa mchezo wa ngumi kusikika wakilia kuomba usimamizi wa serikali katika mchezo wa ngumi za kulipwa.
Licha ya jitihada za wadau kupambana na kuhakikisha ngumi zinafikia mahali panapo vutia  lakini bado kumekuwa na matatizo kila kukicha.
Tatizo kubwa ni watu kujiendesha bila ya kuwa na usimamizi wenye mamlaka kutoka chumbo cha juu  kinachosimamia michezo nchini.
Baada ya kutokea hayo kwa takribani miaka 20, Serikali ya Rais  DR.John Magufuli imekuja na mkakati wa kuwaundia chombo cha kutengeneza sera na kanuni za kuusimamia mchezo huo wa ngumi za kulipwa nchini.
Kamati hiyo inayoundwa na watu Sita iko chini ya Mwenyekiti Habibu Kinyogoli  Katibu mkuu kwa sasa ni Chaulembo Palasa baada ya Emanuel Mlundwa kusimamishwa kufanya kazi za masumbwi nje na ndani ya nchi.
Kamati ilipata baraka za Katibu wa baraza kwenda kuandaa miongozo na kanuni za kusimamia ngumi za kulipwa nchi nzima.
Kinachostaajabisha watu hawa baada ya kupewa uhuru wa kujichaguwa wakatumia uhuru huo kujipanga wao wenyewe huku wakijuwa kati yao hakuna maelewano.
Mlundwa ambae alikuwa katibu wa kamati hiyo hana maelewano mazuri na katibu wa sasa Chaulembo Palasa mpaka kufikia kupelekana mahakamani.
Historia inaonyesha kuwa Mlundwa ndie aliyempa Chaulembo pesa na wakiri wa kusimamia  kesi iliyokuwa imefunguliwa na Onesmo Ngowi baada ya Chaulembo kuwa akimfanyia visa katika shughuli zake.
Dhumuni la kumpa pesa hiyo ilikuwa ni kumuondoa Ngowi kwenye Uwenyekiti kwa sababu kulikuwa na mwingiliano wa kimaslai kati yao.Hivyo akichukuwa Chaulembo, Mlundwa atakuwa huru kufanya biashara zake.
Cha kushangaza baada ya Chaulembo kushinda kesi uadui ukahama kutoka kwa Ngowi ukaja kwa mtu aliyemuweka yeye mwenyewe.
Kutokana na historia hiyo mvutano kati ya Mmiliki wa kampuni ya Puglistic Syndicate of Tanzania (PST) na Tanzania Professional Boxing Commition (TPBC), umeendelea kuwa kikwazo katika mchezo wa ngumi za kulipwa nchini.
Baada ya mpasuko huo Serikali kwa kupitia Waziri wa Michezo Nape Nauye aliamuwa kuwaita wahusika wote wa Makampuni na Chama ili kutaka kuweka mambo sawa.
Chakushangaza ndani ya kamati hiyo iliyopewa kazi kwa miezi kadhaa tayali kunampasuko,mpasuko huo unakuja baada miongoni mwao wanaounda hiyo kamati wanamgongano wa kimaslai.
Juzi aliyekua katibu wa kamati hiyo Emanuel Mlundwa alijikuta kwenye kashfa ya kuwatumia watoto wadogo waliochini ya miaka 18, katika mchezo kati ya Thomas Mashali na Sajjad mehrab.
Nikweli watoto walitumika kinyume na taratibu maana hakuna sheria inayoruhusu watoto kuwa eneo la starehe mpaka usiku wa Saba na pia kuwatumia katika ngumi za kulipwa.
Wakati  huo tayali alikwisha andikwa na  Baraza la michezo yenye kumbukumbu namba- KVJM/MIC/SR/1/28/87 iliyokuwa ikimtaka  ajieleza kwanini asichukuliwe hatu kwa kuwachezesha utangulizi watoto Mawazo Leonard na Mbaraka Ally,  katika mechi ya Monica Mwakasanga Tanzania na Marischa Sijauw wa Uholanzi.
Hivyo kitendo cha kuwatumia watoto katika michezo Mlundwa amezoea ndio maana hakuwa na hofu kuwapandisha tena kwenye ulingo.
Kitendo cha kuwapandisha watoto kwenye ulingo kilitafasiliwa kuwa ni ukiukwaji wa haki za watoto ambazo ni kinyume cha mikataba ya umoja wa mataifa inayokataza ajira kwa watoto.
Chakushangaza Mlundwa anasema Mataifa makubwa yanawatumia watoto katika ngumi za kulipwa ikitolea mfano Cuba na Marekani.
Tukio hilo lilifanya vyombo vya habari kumtaka Yasin Abdallah (Ustadhi) mmiliki wa Kampuni ya Tanzania Boxing Proffesional Organisation (TPBO) kutolea ufafanuzi suala la kutumia watoto katika ngumi za kulipwa.
Ustadhi alitolea ufafanuzi kuhusiana na hilo kuwa nimakosa kuwatumia watoto kwenye mchezo wa ngumi za kulipwa na ni hatalishi kwa afya zao na malezi kwa ujumla.
Lakini Mlundwa alikuja juu na kumtolea lugha chafu Yasin Abdallah (Ustadhi) kitu kilichoibuwa mtikisiko kati ya wadau wa ngumi na kupelekea wadau hao kukutana wiki moja baadae.
Mlundwa alisema sio ajabu kuwatumia watoto kwenye ngumi za kulipwa kwani mataifa makubwa yanawatumia katika huu mchezo.
Swali la kujiuliza kama Mlundwa anasema Mataifa makubwa yanawatumia watoto katika ngumi za kulipwa,sisi tanzania tunafuata Sheria gani ya kimataifa?
Ukichunguza kwa undani utagunduwa kuwa Mlundwa ni wakala wa kutekeleza Sheria, Kanuni na Sera za mataifa ya ulaya, ambazo hapa kwetu bado hatujaanza kuzitumia na pengine tusizitumie.
Mlundwa alienda mbali zaidi kwa kusema kama yeye amewatumia watoto na kila mtu ameona anaomba atua zichukuliwe dhidi yake lakini hao wanaomshambulia kwa kufanya vikao anaomba wasitumie kisingizio cha watoto kumziba mdomo asiseme siri zao.
Alisema wanaomchafuwa ni wale wote ambao wamekuwa na utaratibu wa kupeleka mabondia nje huku wakiwa sio mambondia na kuishia huko huko.
Mludwa alisema miezi michache iliyopita Chaulembo Palasa alitoa vibali kwa bondia watatu, na mtu mmoja ambae si bondia ambae alitambulishwa kwa hao mabondia kuwa ni Meneja wao.
Mbali na ayo Mlundwa alisema kama wao ni wasafi kwanini hawatoi maelezo ya kwanini Shomari Kimbau alirudia uwanja wa Ndege nchini Urusi, nini kilimfanya arudi ikiwa kila kitu kiliratibiwa huku Dar es salaam
Mwandishi wa makala hii hakuishia hapo aliamuwa kumtafuta Rais wa TPBC Chaulembo ili aseme huyo mtu mmoja aliyebaki Russia ni nani na kwanini Meshack Mwankemwa waliishia uwanja wa ndege Urusi alipopatikana alisema hajui hizo taarifa na anamshangaa Mlundwa kusema kunamtu kabaki Rusia.
Lakini pia suala la Kimbau na Mwankemwa kurudia uwanja wa Ndege lilitokana na Shomari kutokuwa na mawasiliano mazuri na promota wa mechi ya mwankemwa.
Embu tujiulize mtu anawezaje kutoka Tanzania mpaka Urusi bila kuwa na mawasiliano na mwenyeji wake, je hizo nyaraka walizopeleka ubalozini ili wapewe kibali cha kukaa Urusi zilikuwa hazionyeshi tarehe,mwenyeji wao na dhumuni la wao kwenda kule?
Mbali na hayo kawaida ya ngumi za kulipwa ukishakuwa na mchezo lazima utaonekana kwenye ubao wa matangazo wa kimataifa (Box rec) na ukweli mchezo wa Mwankemwa ulikuwa unasoka tarehe usika.je nini kilitokea akaishia uwanja wa ndege.
Ukiangalia kwa kina utaona kunauondokaji wa kiholela wa watanzania kwenda nje, je safari za mabondia hawa Ofisi za uhamiaji wanapata taarifa au nao huwa wanaacha watu wajiondokee hasa mabondia.
Kutokana na mlolongo huu uliojaa ubabaishaji mwandishi wa makala akapiga hodi Ofisini kwa Katibu wa baraza la MichezoAbdallah Kiganja.
Mwandishi: Ndugu Kiganja unafahamu nini kuhusiana na huu mvutano wa Kamati ya kuunda katiba ya kusimamia ngumi za kulipwa.
Kiganja: Sijapata taarifa yoyote inayohusu hii kamati iliyoundwa.
Mwandishi: Hunataarifa za Emanueli Mlundwa kutumia watoto katika mchezo wa mashali Sajjad mehrab?
Kiganja:Sina taarifa kuhusiana na ule mchezo maana sikuwepo Ofini nilikuwa safarini.
Mwandishi: Sheria za nchi kwenye masuala ya michezo inawataka watoto washiriki michezo mpaka saa ngapi?
Kiganja: Watoto mwisho saa 12,jioni,wanapaswa kuwa wamemaliza michezo yao.ikitokea wameshirikisha watoto katika michezo yao basi wazingatie taratibu zinataka nini.
Ikitokea ikadhibitika waliwatumia watoto katika mchezo ule  Baraza litachukuwa hatua kwa wale wote waliohusika katika kuwatumia hao watoto.
Kutokana na maelezo ya kiganja anapenda michezo ishirikishe watoto lakini izingatie kanuni.Je kwa  matumizi yale ya mtoto wa kike (Red Card) je ni utaratibu upi mpaka usiku wa saa Saba?
Ifikie mahali sasa Serikali ionyeshe makucha yake kwa watu wa mchezo wa ngumi maana wamejisahau wanajiendesha wanavyojisia.
Sio ajabu kusikia Gloves zikatumiwa na wachezaji wote,sio ajabu kuona watazamaji wakilaani maamuzi mabaya yanayotolewa na waamuzi wakati wa mchezo,sio ajabu kuona bondia anashuka  ulingoni hajavishwa mkanda kisha kujibiwa "Mkanda hata mbwa anao".
Kama serikali imeshindwa kudhibiti huu mchezo bora iufute ili kutoa nafasi ya kujipanga upya kuliko kuuwacha ubaki kuwa wa watu binafsi.
Huwezi kusema eti umeunda kamati ya kuandaa katiba huku walioteuliwa ndio wamiliki wa haya makapuni yaliyotufikisha hapa mbali ya kuwa wao wenyewe hawaelewani kila siku malumbano.
Tusipokuwa makini kwenye hili watamponza Waziri wa Michezo atumbuliwe kwa sababu ya njaa na uhasama wa kati ya wamiliki wa haya makampuni na chama.
hata hivyo mimi binafsi napendekeza kuwe na chombo kitakacho ratibu mchezo wa ngumi za kulipwa kwapamoja ili kusiwe na mgongano na migogolo kwa watendaji wake ila chombo kitoe ruhusa kwa mawakala wa mchezo wa ngumi kutafuta michezo mingi zaidi nje a nchi ili mabondia wapate kunufaika na mchezo wauchezao wakati wangali na nguvu zao

ni siwe mwingi wa maneno kwa leo naomba kuishia hapo ili utaratibu na maamuzi ya busara ufuate mkondo wa uongozi wa pamoja

Post a Comment

0 Comments