Tamasha la filamu la Zanzibar (ZIFF) limetangaza majina ya filamu
zitakazoshindanishwa hapo ifikapo Julai 9 hadi 17. Tamasha lilipokea jumla ya
filamu 490 kutoka nchi 32 mwaka 2016.
Jopo la wachaguzi limependekeza filamu 80 ndio zitakazoshindanishwa
katika makundi matano maalum: Kundi la Kawaida 59, Sembene Ousmmane 15, filamu
12 Bongo movies. Nyingine 5 ni la kundi
jipya kabisa la filamu zinazoizungumzia Zanzibar itakayopata tuzo ya Emerson.
Kutakuwepo pia mashindano ya Video za Muziki ambazo zitatangazwa mwisho
wa mwezi Mei na hizi zitaoneshwa katika maonyesho yanayofanyika katika Ngome
Kongwe.
Jambo la kukumbukwa zaidi mwaka huu nikuongezeka kwa jumla ya filamu za
kitanzania katika mashindano. Filamu zaidi ya 40 zilitumwa kwa mashindano kwa
ujumla na mwaka huu filamu 5 za kitanzania zitashindanishwa katika jopo la
Ousmane Sembene kati ya filamu 17.
Kwa ujumla filamu toka Afrika mashariki zinazoingia katika mashindano
zimeongezeka pia ambapo kuna 8 toka Tanzania, Kenya 5, Uganda 3 na Rwanda 2.
Mwaka huu kutakuwa na filamu 3 ambazo zitaoneshwa kwa mara ya kwanza
duniani katika tamasha la ZIFF. Filamu
hizi zimedhaminiwa na Shirika la Ushirikiano wa Kimataifa la Ujerumani (GIZ)
wakishirikiana na ZIFF. Washindi watatu wa shindano la Sembene Ousmane mwaka
2015 walipewa $2000 kila mmoja kuwawezesha kutengeneza filamu mpya katika
kipindi cha mwaka na kuzituma tena ZIFF kwa kushindanishwa na nyingine.
Mvuto wa tamasha unazidi kukua ukiangalia kuongezeka kwa nchi
zinazotuma filamu. Mwaka huu Estonia na Albania zimetuma filamu zikiungana na
nchi nyingine kama Bangladeshi, Finland, Trinidad and Tobago, Bermuda na
nyinginezo.
ZIFF pia inaendeleza mchango wake katika tasnia ya filamu kwa
kutayarisha warcha maalum juu ya utengenezaji filamu. Mwaka huu ZIFF imetangaza
warsha mbili. Ya kwanza ni juu ya matumizi bora ya Camera ya Canon D5
itakayoendeshwa na Barry Braverman toka Marekani ,aliyeifanyia kazi Panasonic
na Sony katika kujaribisha vifaa vyao.
Warsha nyingine ni ile itakayodhaminiwa na Goethe Institute ya
Ujerumani itayofunza watoto wa shule ufundi wa kutengeneza vikaragosi katika
filamu. Hii inatokana na kutambua nafasi ya sanaa katika kukuza vipaji na
kuwatayarisha watoto wasanii kwa ajira, uadilifu na ubunifu.
Kwa maelezo zaidi na kupata listi ya filamu zilizochaguliwa tembelea
tovuti ya www.ziff.or.tz na pia tafadhali tu-like katika Facebook
0 Comments