Sisi Wanamtandao wa Wanawake na Katiba/Uchaguzi na Uongozi tumesikitishwa na kufadhaishwa sana na hali ya udhalilishwaji na matumizi ya lugha chafu na za kejeli dhidi ya Wanawake Bungeni. Kauli kama hizi zinaendeleza dhuluma, udhalilishaji ana kuwanyima wanawake haki yao ya kikatiba na kuwakosea heshima.
Kilichotokea Bungeni hivi karibuni na ambacho kimekuwa ni muendelezo wa matukio ya utumiaji wa lugha ya kudhalilisha wanawake bungeni na wanawake wote nchini ni kitendo ambacho hakitavumiliwa na kufumbiwa macho na wale wote, na hasa wanawake, ambao wana nia ya dhati ya kujenga uwiano wa kijinsia katika ngazi za uongozi nchini.
Tukio hili ni kinyume na Tamko la Kimataifa Kuhusu Haki za Binadamu (UDHR:1948) Mkataba wa Kimataifa wa Kutokomeza aina zote za Ubaguzi dhidi ya Wanawake (CEDAW: 1979, na mikataba mingine ya Haki za Binadamu na Usawa wa Kijinsia ambayo nchi yetu imeridhia. Aidha ni kinyume pia na Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (1977) Ibara ya 9(f),(g) na (h) na Ibara ya 12 (2) pia ni uvunjwaji wa sheria namba 15 ya mwaka 1984 ib. 6.
Ni katika muktadha huu, tunakemea na kulaani vikali mwenendo huu ambao unarudisha nyuma harakati za kutetea haki za wanawake katika uongozi na kukiuka misingi ya utawala bora nchini.
Ikumbukwe kuwa Bunge ni nguzo na muhimili mmojawapo mkuu katika nchi hii. Hivyo basi Bunge halipaswi kuruhusu mbunge yeyote yule (awe wa kiume au wa kike) kutumia chombo hiki muhimu kukandamiza sauti za wanawake bungeni na kuwaondoleaa hadhi ya utu wao ili wasijiamini katika uongozi na hivyo washindwe kutetea maslahi ya watanzania.
Aidha sisi wanamtandao tunataka kuona hatua stahiki za kinidhamu zinachukuliwa dhidi ya wale wote wenye tabia kama hizi ili kukomesha mwenendo huu. Hali kadhalika tunatoa wito kwa jamii kwa ujumla kukemea na kuwawajibisha wabunge wao ambao wamewapa kura ili wakatetee maslahi ya kimaendeleo kwa wananchi wote (wanawake na wanaume).
Imetolewa na:
Lilian Liundi – Mkurugenzi Mtendaji TGNP
Kwa niaba ya; Women Fund Tanzania, Tanzania Women Lawyers Association, TAMWA, TWCP-ULINGO
11/05/2016
NMB YATOA MSAADA WA VIFAA VYA SH. MIL. 23 KATIKA SHULE 3 MUFINDI
-
Benki ya NMB imetoa msaada wa mabati 150 na madawati 150 kwa shule za
msingi KASANGA, KISASA na SAWALA zilizopo wilayani Mufindi mkoani Iringa
vyenye thama...
1 hour ago
0 Comments