NA MWANDISHI WETU, MAELEZO
SIKU chache baada ya shindano la kumsaka Mrembo wa Tanzania kutoka kwenye kifungo cha Baraza la Sanaa la Taifa (Basata) uongozi wa Hashim na wenzake wameachia ngazi kupisha uongozi mpya wa mpito.
Akizunguma leo asubuhi katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika
kwenye ukumbi wa mikutano wa Idara ya Habari (MAELEZO), Jijini Dar es Salaam Mkurugenzi wa Kampuni
ya Lino International ambaye pia alikua
Mratibu kwa kipindi cha miaka 21 Hashi Lundenga alisema , “tumekuja hapa
leo ikiwa ni katika kutangaza majina mapya ya Kamti ya Miss Tanzania ambao
kuanzia sasa watakuwa wakiratibu shindano hilo.
Sisi
tutakuwa nyuma yao hivyo anomba
waandishi wa habari muendelee kuwapa ushirikiano wa kutosha.
Lundenga
aliitaja kamati hiyo kuwa ni majina na cheo kwenye mabano Juma Pinto
(Mwenyekiti wa muda) na Lucas Rutta (Makamu wa Mwenyekiti), Doris Mollel (Katibu Mkuu) na Jokate Mwegelo (Msemaji wa
Kamati),
Wengine ni
katika nafasi ya wajumbe ambao aliyekuwa Miss Tanzania 1999 Hoyce Temu,
Mohammed Bawazir, Gladyz Shao, Shah Ramadhan, Hamm Hashim , Khalfan Saleh na
Ojambi Masaburi.
Aidha kwa
upande wa sekretarieti wamowajumbe wanne ambao ni Dk. Ramesh Shah,
Hidan Ricco aliyekuwa Ofisa Habari wa Lino, Yasson Mashaka na Deo
Kapteni.
“Hii ndiyo
timu yetu ya wachapa kazi ambao
tumewakabidhi jukumu hili la kuandaa,
kusimamia na kuratibu mashindano ya
urembo ya Miss Tanzania.
Akizungumza
mara baada ya kutangazwa majina hayo Pinto alisema kwamba anahidi kulibadilisha
shindano hilo ambalo linapendwa na wengi hivyo amehitaji muda ili waweze
kujipanga ikiwemo hatma ya ushiriki wa Miss Tanzania Lilian Kamazima kwenye
fainali za shindano la kumsaka mrembo wa dunia zitakazo fanyika nchini China
baadaye mwaka huu.
“Suala la
kushiri kwa mrembo wetu tutalitolea ufafanuzi baada ya wiki mbili pia nina
imani majibu yatakuwa mazuri siku ikifika” alisema Pinto.
Jibu hilo la
pinto lilikuja baada ya kuulizwa hatma ya ushiriki wa Miss Tanzania ambapo
Lundenga alikiri kwamba hawataweza kumuanda kutokana na kuwa nyuma ya muda wa
maandalizi pamojana na ukosefu wa fedha pia.
Pinto
aliendelea kwa kusema kwamba ndiyo kwanza wamekabidhiwa ofisi leo hivyo
wanahitaji kukaa ofisini na kukabidhiwa
rasmi ndipo watajua wapi pa kuanzia.
Wakati
huohuo Mwegelo alizungumza kwamba anampongeza Lundenga kwa kukubali kuachi
kituia mbacho amekitumikia kwa muda mrefu kwani siyo jambo rahisi.
Pia
aliongeza kwa kusema kuwa watakutana na Basata ili waweze kuzungumza na
kufahamishana lipi la kufanya na lipi wasilifanye
na baada ya hapo ndipo watakapotoka na uamuzi kama shindano lifanyike mwaka huu
ama wasubiri hadi ifikapo mapema mwakani.
Pia ametoa
wito kwa wasichana ambao walipoteza matumaini na imani ya mashindano ya urembo
kwa kusema kuwa anawatoa hofu kwani hakuna
jambo lililoharibika hivyo wakati ukifika wajitokeze kwa wingi.
“Natoa wito
kwa wasichana kuwa waondoe hofu kwani hapa wako kwenye mikono salama” alisema.
Viongozi wa
Lino ambao umelazimika kupisha na kufanya mabadiliko ni pamoja na aliyekuwa
wake Katibu Bosco Majaliwa,
Mkuu wa Itifaki Albert Makoye, Hidan Rico
Ofisa Habari na Yasson Mashaka aliyekuwa Mjumbe.
0 Comments