TAASISI ya Kuzua na Kupambana na Rushwa nchini (TAKUKURU) Mkoa wa Pwani leo tarehe 21 Januari 2026 imekabidhi vifaa tiba vya kisasa vya aina mbili tofauti kwa ajili ya kusaidia ukuwaji wa watoto njiti,katika Hosptali ya Rufaa ya Mkoa wa Pwani Tumbi.
Akikabidhi msaada huo katika
Hosptali hiyo Mkurugenzi wa Taassii ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini TAKUKURU Crispin Chalamila ambaye alikuwa mgeni rasmi kwenye hafla ya makabidhiano hayo amesema kuwa msaada wa mashine hizo umetolewa kwa michango ya hiayari iliyotolewa na wafanyakazi wa Taasisi hiyo ikiwa ni katika lengo la kuunga mkono jitihada za serikali za kupunguza vifo vya watoto njiti nchini.
Mkurugenzi Chalamila amesema kuwa msaada huo ni muendelezo wa misaada inayotolewa na Taasisi hiyo katika Hospitali mbalimbali nchini.
"Watumishi wa TAKUKURU kwa pamoja tulikubaliana tutoe sehemu ya mishahara yetu kama michango ili kufanikisha ununuzi wa mashine hizi na mpaka sasa tumekwisha toa katika
Hosptali nane katika mikoa nane nchini"amesema.
Aidha Mkurugenzi huyo wa TAKUKURU amesema lengo la Taasisi hiyo ni kuendelea kutoa michango hiyo katika Hosptali zote nchini ambapo ametoa wito kwa Taasisi nyingine za kiserikali na watu binafsi nchini kusaidia jitihada za serikali katika kupambana na vifo vya watoto wachanga.
Wakati huohuo Kamanda wa TAKUKURU Mkoa wa Pwani Domina Mkama amesema wamekuwa wakishirikiana na Hosptali hiyo katika masuala mbalimbali ikiwemo utoaji wa elimu za rushwa na Afya.
Kwa upande wake Mganga Mfawidhi wa Hosptali ya Rufaa ya Mkoa wa Pwani Tumbi Dkt. Amani Malima amesema kuwa anatoa shukrani kwa niaba ya Hospitali hiyo kwa msaada uliotolewa na Taasisi hiyo ni muhimu kwa usawi na ukuwaji wa watoto njiti na kwamba watahakikisha wanatunza vifaa hivyo."Natoa rai kwa Taasisi zingine za serikali wake watoe misaada ya vifaa mbalimbali kwani bado tuna mahitaji mengi .
Dkt. Adelina Rutashobya ambaye ni Darktari wa Watoto katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Pwani Tumbi amesema kuwa katika kipindi cha mwaka 2025 walipokea jumla ya watoto 1,393 ambapo kati yao 370 walizaliwa kabla ya wakati sawa na asilimia 27% na kwamba watoto 173 waligundulika na magonjwa ya moyo na 61 wamefariki.
"Asilimia kumi (10%) ya watoto hao walipewa rufaa na asilimia 80.8% waliruhusiwa lakini pamoja na mafanikio machache changamoto inayotukabili ni ukosefu wa vifaa tiba na dawa kwa ajili ya watoto njiti"amesema Dkt. Rutashobya.
Amesema kuwa upungufu wa vifaa hivyo ni pamoja na mashine za uangalizi wa karibu za watoto, mashine za maji pamoja na dawa za kukomaza mapafu ya watoto.









0 Comments