Rais
Jakaya Kikwete (kulia) akimkabidhi Mkurugenzi Mkuu wa Kiwanda cha
Tanzania Distilleries Limited (TDL), maarufu kwa jina la Konyagi . David
Mgwassa Kombe la ushindi wa mwaka wa uzalishaji bora nchini katika
hafla ya Shirikisho la Wenye Viwanda nchini (CTI) Jijini Dar es
Salaam.Mwandishi Wetu
MKAKATI
wa kumng'oa Mkurugenzi Mtendaji wa Kiwanda cha Konyagi (TDL) David
Mgwassa umebainika kutokana na kuwepo kwa njama zinazoendeshwa kwa siri
na makaburu.
Uchunguzi
uliofanywa na mtandao huu umebaini kuwa kiongozi huyo amekuwa akipigwa
vita kutokana na kile kinachoelezwa kuwa ni mafanikio yanayopatikana
chini ya uongozi wake.
Makaburu
hao wamekuwa wakifanya njama mbalimbali za kumng'oa kwa kile
kinachodaiwa kuwa ni kutaka kushika wadhifa wa mkurugenzi huyo kwa kutoa
taarifa ambazo si za kweli kwa uongozi wa ngazi za juu nchini Afrika
Kusini na Uingereza.
Kwa mujibu wa chanzo chetu cha habari kimeeleza kuwa kiongozi huyo ametakiwa kukabidhi ofisi ifikapo Julai 30, mwaka huu.
Chanzo
hicho kimeeleza kuwa tayari taarifa za kuondolewa kwa kiongozi huyo
zimezagaa katika viwanda vya TDL na Kiwanda cha Bia Tanzania (TBL) pia
tangazo la kumbadilisha limetolewa kupitia kwenye mtandao wa kijamii wa
WhatsApp na kutangaza Kenya na Uganga.
Kutokana
na taarifa hizo baadhi ya wafanyakazi wa kiwanda cha TDL wameazimia
kugoma ili kushinikiza mkurugenzi huyo kuendelea na madaraka yake.
"Tumesikia
taarifa kuwa mkurugenzi wetu anaondolewa madarakani kwani tumeshangazwa
sana kutokana na kuishi naye vizuri na kupatikana kwa mafanikio mengi
tangu ashike wadhifa huo na pia ameboresha maisha yetu kwa kutuongezea
mishahara," alisema mfanyakazi mmoja ambaye hakutaja jina lake kuandikwa
gazetini kwa kuwa si msemaji wa wafanyakazi.
Hata hivyo kuna taarifa kuwa Bw. Michael Benjamin anatarajia kushika wadhifa wa Bw. Mgwassa.
Mtandao
huu ulimtafuta Mkurugenzi wa Uhusiano na Sheria wa Kampuni ya Bia
Tanzania (TBL). Steve Kilindo ili kuzungumzia taarifa hilo alikiri
kuwepo kwa mabadiliko hayo lakini hana taarifa zaidi kuhusiana na sakata
hilo.
"Kweli kuna mabadiliko hayo ya uongozi lakini taarifa za ndani sina," alisema.
Mike Benjamin kutoka Afrika Kusini anayetarajia kurithi cheo hicho
0 Comments