MWANAMUZIKI mkongwe nchini
Ramadhani Masanja ‘Banzastone’ amefariki dunia nyumbani kwao Sinza njia panda
Lion jana mchana baada ya salat Jumaa.
Banzastone amefariki dunia
baada ya kuugua kwa muda mrefu huku
akipelekwa hospitali na kutibiwa nyumbani kwa tiba za aina mbalimbali.
Taarifa rasmi za kifo cha mwanamuziki
huyo zilitolewa jana na kaka yake Khamis Masanja .
Masanja alisema kwamba kifo cha Banzastoner kimekuja baada ya kuugua
kwa muda mrefu ambapo alikuwa akisumbuliwa na kifua pamoja na fangas za
kichwani.
Aidha kaka huyo wa marehemu alisema
kwamba taratibu za mazishi zinafanyika kwa kuzingatia familia yao ilivyokua
kubwa hivyo taarifa zaidi zitatolewa
hapo baadaye.
Naye
Mkurugeni wa Kampuni ya The African Stars Entertainment (ASET)Asha
Baraka alisema kwamba amepokea kwa majonzi makubwa taarifa za msiba huo kwani
yeye amekuwa katika mstari wa mbele
katika kupigania uhai wa mwanamuziki huyo aliyekuwa mahiri katika utunzi na
kuimba pia.
Itakumbukwa kwamba Banzastone
ni kati ya wanamuziki waasisi wa bendi ya Twanga Pepeta ambapo pia atakumbukwa
kwa kuachia vibao kadhaa ikiwemo Kumekucha, Aungurumapo Simba, Mtu Pesa, na
wimbo wake mmoja ambao aliuachia wakati akiwa na bendi ya Twanga Chipopolo aliachia wimbo wa ‘Hujafa
Hujasifiwa’ ambao katika mashairi yake alijiimba yeye mwenyewe huku akisema
siku akifa atasifiwa sana wengine watamwita Teja na mambo mengi alizungumza
katika wimbo huu.
Mapema mwezi huu Banzastone alilazwa katika Hospitali ya
Mwananyalama , Kinondoni Jijini Dar es Salaam kabla ya kupata ruhusa ya kurudi
nyumbani. shughuli za msiba zitakuwa nyumbani kwao Sinza njia panda Lion Jijini Dar es Salaam.
0 Comments