Na Zawadi Chogogwe
MKUU wa Wilaya ya Kinondoni,
Paul Makonda, amesema Tanzania haina tatizo la ajira ila kuna tatizo la fikra.
Makonda alitoa kauli hiyo, mwishoni
mwa wiki wakati wa uzinduzi wa maonyesho ya tano ya Tanzania Homes Expo yaliyoandaliwa na Kampuni
za EAG Group jijini Dar es Salaam.
Alisema Tanzania ina
rasilimali nyingi lakini vijana wamekuwa hawazioni fursa ambazo zingeweza
kuwapatia ajira na kuondokana na
kuilaumu Serikali.
“Tanzania ina rasilimali
nyingi ambazo kama vijana
wangezitumia zingeweza kuwapatia ajira na kuondokana
kukimbilia nchi jirani kujihusisha na uuzaji wa dawa za kulevya na
kuishia kutofikia malengo yao.”alisema Makonda.
Alisema fursa hizo zimekuwa
zikichangamkiwa na wageni ambao wanatengeneza malighafi kwa kutumia rasilimali
za hapa nchini.
“Vijana wengi wanakimbilia
nje ya nchi wanaziacha fursa na kushindwa
kukuza uchumi wa nchi” alisema Makonda.
Kwa upande wake Mkurugenzi
Mkuu Mtendaji wa Kampuni za EAGgroup, Imani Kajura, alisema maonyesho ya Tanzania
Homes Expo lengo lake ni kutoa elimu kwa jamii ili ielewe masuluhisho mbalimbali ya makazi yao.
Kajura aliongeza kuwa lengo
kubwa la Tanzania Homes Expo ni kuweka jukwaa moja la mtu anayetafuta
masuluhisho ya nyumba kuanzia Ulinzi na kudai kuwa Watanzania wengi hawajui njia za
kuweka maeneo yao ya makazi yakawa katika hali ya usalama
“Jinsi Nchi yetu inavyozidi
kukua, kunakua na watoa huduma mbalimbali kwa upande mmoja kuna wahitaji
huduma upande mwingine, kwenye sekta ya makazi tukaona ni muhimu kuwa na sehemu
ambayo watoa huduma na wahitaji huduma
wanakutana kwa pamoja.
Maonyesho haya yanashirikisha
washauri wa masuala ya ujenzi, wajenzi wa majengo na nyumba za kuuza, kampuni
za bima, wanaoendeleza viwanja, Kampuni za fedha pia suala la Afya lipo.”alisema
0 Comments