Mwanamuziki wa muziki
wa kizazi kipya, Aboubakar Katwila ‘Q-Chief’ picnani juu, amesema anamshukuru Mungu amerudi tena katika wigo wa muziki wa
kizazi kipya huku akipania kufanya makubwa.
Q-Chief alisema hayo
jana wakati akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika kwenye
Ukumbi wa Mikutano wa Idara ya Habari
(MAELEZO), jijini Dar es Salaam.
Msanii huyo ambaye
alipotea katika anga ya muziki kwa muda, amesema licha ya kuwa kwake nje ya
muziki kwa muda mrefu, yupo vizuri kwani alikuwa akisoma na kuangalia soko
linahitaji kitu gani.
Aidha, leo anatarajiwa
kuzindua albamu zake mbili alizorekodi nchini Afrika Kusini, akisema ni zenye ubora
wa hali ya juu na kuwasihi mashabiki wampokee kwa mikono miwili.
Chilla amesema hivi
sasa amerudi katika fani huku akimuahidi Meneja wake, Mhonda kuwa atakuwa na
nidhamu, mchapa kazi na mapito yake yote ya zamani ambayo alikumbana nayo
mashabiki wasimhukumu, wamuangalie Chilla wa sasa.
Chilla leo jioni Alhamisi atakuwa na sherehe fupi ya
kutambulisha video zake mbili ambazo
amezirekodi nchini Afrika Kusini katika
Hoteli ya City Style na baada ya hapo
atakusanya maoni kutoka kwa wadau kuhusu video zake mbili ambazo ni ‘For You’
na ‘Power of Love’, ambazo amezitengeza chini ya uongozi wa Apex Group of Companies Limited huku akisimamiwa na Meneja Julius Mhonda.
Mhonda aliweka wazi
kwamba yeye hana anachotegemea kupata kutoka kwa Chilla, kwani anamsaidia tu,
hiyo ni kutokana na kuona kipaji cha msanii huyo kikipotea, hivyo ameamua
kumsimamia ili arudi katika chati kwani yeye anafurahi kuona kwamba anasaidia
wasanii ili waweze kutimiza njozi zao na hayuko kwa wasanii kwa sababu ya
fedha.
Chilla alitoka na
wimbo ambao aliihusisha familia yake, ambapo aliweka wazi maisha ya familia
yake na kutoka na wimbo ambao ulitamba sana ‘Si ulinikataa’, ambapo ilidaiwa
alimuimba baba yake mzazi.
0 Comments