IKIWA
ni siku moja tu baada ya kutokea kifo cha Msanii Chigwele Che Mundugwao (48) pichani kulia Baraza
la Sanaa la Taifa (Basata) wametuma salamu za rambirambi za msiba huo na kusema
wamepokea kwa masikitiko na majonzi makubwa kifo cha msanii wa muziki wa asili
Chigwele Che Mundugwao kilichotokea katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili
Jijini Dar es Salaam leo Asubuhi ya Alhamisi 16 Aprili mwaka huu baada ya
kuugua kwa muda mrefu.
Katika
taarifa iliyotumwa kwa vyombo vya habari na kusainiwa na Katibu Mkuu Godfrey
Mngereza ilimwelezea marehemu Che
mundugwao kuwa alikuwa msanii wa muziki wa asili na mdau wa muda
mrefu katika sekta ya sanaa nchini.
Pia
Che atakumbukwa kwa kuwa na mchango
mkubwa katika kukuza muziki wa asili nchini na baadaye kupitia Chama cha Muziki
wa asili (TAFOMA) nchinijinsi alivyoshiriki
kikamilifu kwenye mchakato wa uanzishwaji wa Shirikisho la Muziki nchini ambalo linaviunganisha vyama vya wasanii
wanamuziki.
Mchango
wake katika muziki wa asili na katika kujenga mfumo wa utawala wa wasanii nchini
hautasahaulika kamwe. Ni mdau aliyeacha misingi katika sekta ya muziki na
amejitolea kwa kiasi kikubwa katika kuufikisha muziki huu mahali ulipo leo.
Baraza,
wasanii na wadau wote wa sanaa hatuna budi kuendelea kuenzi mema yote
aliyotuachia marehemu Che Mundugwao hasa katika kupenda kujitolea muda mwingi
kufanikisha ufanisi kwenye sekta ya sanaa.
Baraza
linatoa pole kwa ndugu wa marehemu, shirikisho la muziki, wasanii na wadau wote
wa sanaa kwa msiba huu. Marehemu amezikwa jana saa kumi alasiri katika makaburi
ya Tegeta.
Mkurugenzi
wa bendi ya Kilimanjaro Waziri Ally alisema kwamba kwa upande wa wasanii
wapepata pigo na pengo ambalo halitaweza kuzibika kwani tangu alipomfahamu Che alikuwa ni mwanamuziki
wa asili na aliyewekeza katika muziki wa asili tofauti na wasanii wengine ambao
wamekuwa wakihamahama katika namna ya upigaji wa muziki.
‘Wengi
tunaelekeza kuwa tunaelekeza hisia zetu nje kabisa ya tamaduni zetu hivyo
wasanii kama Che ni wachache lakini yeye alikuwa ni moja kwa moja muziki wake
ulikuwa ni wa kiasili zaidi na ulibaki
katika asili alifanikiwa kudumisha utamaduni ambao wengine walishindwa” alisema
.
Mwanmuziki huyu aliweza kung’ara hta nje ya mipaka ya nchi hasa katika nchi za ukanda wa Scandinavia ambako alikuwa akipata mialiko mara kwa mara huku wakati mwingine akiwa anakwenda kufanya maonyesho yeye mwenyewe na wakati mwingine alikua akienda na bendi yake ya Mbega Arts iliyokuwa na maskani yake Wilaya Bagamoyo Mkoani Pwani.
Mwanmuziki huyu aliweza kung’ara hta nje ya mipaka ya nchi hasa katika nchi za ukanda wa Scandinavia ambako alikuwa akipata mialiko mara kwa mara huku wakati mwingine akiwa anakwenda kufanya maonyesho yeye mwenyewe na wakati mwingine alikua akienda na bendi yake ya Mbega Arts iliyokuwa na maskani yake Wilaya Bagamoyo Mkoani Pwani.
Waziri
alisema kwamba kila mtu lazima ataonja mauti ila Che ametangulia hivyo wasanii
waliobaki waendeleze .
Hadi
mauti yanamfika alikuwa chini ya ulinzi ambako alikuwa akikabiliwa na kosa la
wizi wa pasi 26 za kusafiria isivyo halali akiwa na aliyekuwa Ofisa Manunuzi wa
Idara ya Uhamiaji Shemweta Kilwasha (31), Mhandisi Idara ya Zimamoto na Uokoaji
Keneth Pius(37) na mfanyabiashra Ally Jabir (34). Che
alikamatwa Aprili 22 2013 Yombo Makangarawe.Pia liwahi
kupata tuzo kadhaa za kuziki wa sili katika tuzo za Tanzania Music Awards
0 Comments