Wanenguaji wa bendi ya Twanga Pepeta waksaidiana kufungua begi alilokuwemo mnenguaji Hassan Mussa 'Super Nyamwela' (PICHA ZOTE NA MICHAEL MACHELA)
Small Nyamwela akitoa shoo mara baada ya kupanda jukwaani.
Choki akipungia mashabiki.
Kalala Junior wakwanza kushoto Choki katikati na Luizer
Luizer akipungia mashabiki hawapo pichani.
Choki na Luizer wakiimba jukwaani
Rapa na muimbaji Kabatano wakiimba pamoja katika onyesho hilo.
Safu ya wanenguaji wa kike wa bendi ya Twanga Pepeta.
Choki akienda sambamba katika kucheza na wanenguaji wa kiume
Wanenguaji wa bendi ya Twanga Pepeta wakiongozwa na Lilian Tungaraza 'Internet' wakinengua na Mtangazaji Isack Gamba huku akiwatunza.
DAR ES ASALAAM
“WALIMWENGU
wabaya walimtesa Chokii..” hivyo ni vionjo alivyoingia navyo
mwanamuziki nguli, Kamarade Ally Choki kwenye onyesho la kumtambulisha
lililofanyika kwenye ukumbi wa Mango Garden Kinondoni jijini Dar es Salaam, juzi usiku.
Baada ya kibwagizo hicho, wapiga vyombo wakazima, kisha
Choki akaimba kibwagizo cha wimbo wake mpya, kilichosema ‘Usiyempenda kaja... usiyempenda karudi chungulia umuone,’ huku
akicheza kwa staili mpya ya kuweka mkono juu ya macho na kubonyea kidogo kama anachungulia.
Choki na wanamuziki wengine wa Twanga, waliimba na kucheza
sambamba huku wakiwaduwaza mashabiki jinsi walivyoonyesha umahiri wao.
Kamarade Choki, ambaye mashabiki walimsubiri kwa hamu kumwona
katika jukwaa la Twanga Pepeta baada ya kurejea, alishangiliwa kutokana na
namna alivyoingia kwa kibwagizo hicho ambacho kinapatikana katika wimbo wake
mpya wa ‘Kichwa Chini’ ambao ni wimbo wake wa 13 ndani ya Twanga.
Licha ya kuwa wimbo huo ulikuwa ni mpya katika masikio ya
mashabiki, lakini ghafla kila mmoja aliyekuwepo aliweza kuimba kibwagizo hicho
kilichoonekana kukamata ghafla mara baada ya wimbo huo kuimbwa na kuomba
urudiwe zaidi ya mara mbili.
Choki alipanda jukwaani saa sita na nusu usiku huku
akiunganisha ngoma zake zote ambazo ziliwakuna ipasavyo mashabiki wengi
waliojitokeza.
Licha ya kuwa na tishio la mvua na manyunyu ya hapa na
pale, lakini mashabiki walianza kuingia ukumbini kuanzia saa moja jioni na hata
ilipotimu saa tatu hadi saa nne watazamaji walioingia walipata usumbufu wa
kutafuta mahali pa kukaa.
Mwanamuziki huyo mwenye mvuto na mashabiki lukuki,
alijitangaza kuwa hivi sasa anafahamika kwa jina la Sir. Cho, jina ambalo
alipewa alipokuwa nchini Japan.
Baada ya kuimba wimbo huo mpya, pia Choki aliimba nyimbo kadhaa
alizoimba miaka ya nyuma kama ‘Password’,
‘Chuki Binafsi’ na nyinginezo, ambako muda wote mashabiki walionekana kupagawa
na kwenda kumtuza.
Akiwa jukwaani, Choki alisema anawashukuru mashabiki na
kuwaomba wajipigie makofi kwa kuja katika shoo ya utambulisho wake.
Katika onyesho hilo,
pia mnenguaji mahiri, Hassan Mussa ‘Super Nyamwela’ alitambulishwa, ambaye
aliingia kwa mtindo wa kubebwa katika sanduku la nguo.
Akiwa ndani ya sanduku hilo, wanenguaji wenzake waliliburuza kwa
matairi na kumpandisha jukwaani bila ya watazamaji kutambua nini kilikuwa
kikiendelea na mara baada ya kulifikisha, wakasema wanatoa zawadi ndipo Super K
alipovuta zipu huku ndani akiwemo Nyamwela na kushangiliwa na mashabiki.
Naye Kiongozi Mkuu wa bendi hiyo, Luizer Mbutu, alitangaza
nafasi za Choki ndani ya bendi hiyo kuwa ni Mkuu wa nidhamu, Kiongozi Mkuu
Mtendaji na Mkuu wa steji.
0 Comments