:
MSANII nguli wa muziki wa kizazi kipya nchini ‘Bongo Flava’ aliyewahi kutikisa
na vibao vya ‘Nakupenda tu’, ‘Mwanangu Hunanidhamu’ , ‘Ni saa ya kufa
kwangu’ na ‘Umeondoka’ Geofrey Tumaini a.k.a ‘Dudu Baya’ pichani kulia mwishoni mwa wiki
Jumamosi Machi 14 alijikuta kwenye
wakati mgumu baada ya kunaswa akiiba
simu .
Tukio
hilo la fedheha lilitokea
usiku wa Jumamosi kwenye ukumbi
wa Mango Garden , Kinondoni Jijini Dar es Salaam , ambapo msanii huyo galacha
licha ya kuwa mbabe lakini alijikuta akilainika na kuinamisha kichwa
chini kutokana na kukutwa na simu ya ‘Pedeshee’
Fredito Mopao.
Dudu Baya
ambaye alikaribishwa kwenye meza ya Mopao na Mpambe mkubwa wa Mopao anayefahamika kwa jina la John Cena , alikaa hapo huku wote wakifurahia
ofa zilizokuwa zikitolewa na Mopao
lakini haikufahamika ni muda upi
msanii huyo alikwapua simu.
Wakati Mopao
alipotaka kuondoka ukumbini hapo ndipo
aliposikika
aking’aka simu yake aina ya Samsung Note4 iko wapi.Wakaanza kuulizana taratibu
katika meza ile lakini hakupata jibu lililoeleweka akaanza kuchachamaa kuidai .
Wakato Mopao
‘akikoroma’ ndipo mtu mmoja alimshuku msanii huyo na kusema
wamsachi miguuni na ndipo simu hiyo ikakutwa imefichwa kwenye soksi.
Wadau
mbalimbali na mashabiki pamoja na Mopao
mwenyewe walitaka kumuangushia kichapo lakini wengine wakatumia busara na
kumwacha msanii huyo akibaki kaduwaa kwa aibu.
Mkurugenzi
Mtendaji wa bendi ya Twanga Pepeta Asha Baraka amesema amesikitishwa sana na
kitendo hicho kwani Dudu Baya alipokelewa kwa heshima zote kama msanii.
“Dudu Baya
ni msanii mkongwe hivyo hatukutarajia kabisa kama angeweza kufanya kitendo cha
fadhaa kama kile hii yote ni tamaa walizonazo wasanii inasikitisha, nina imani
kubwa hata John Cena aliamua kumpeleka katika meza ile maalum ya Mopao kutokana
na heshima yake na mchango mkubwa alioutoa katika muziki wa kizazi kipya katika
sanaa lakini sasa amejiharibia”alisema Asha.
0 Comments