Mke wa Ihhashi akiimba Jukwaani katika tamasha la Sauti za Busara
MSANII
Ihhashi Elimhlope kutoka nchini Afrika Kusini usiku wa
Ijumaaa iliyopita aliweza kukonga nyoyo mashabiki na wadau mbalimbali ambao walifurika
katika tamasha la Sauti za Busara ambazo zilizofanyika kwenye Mji Mkongwe Zanzibar.
Elimhlope
ambaye alitumbuiza sambamba na mke wake pamoja na mtoto wao wa kiume waliimba
na kucheza kwa kutumia lugha ya Xsosa huku mwanzo hadi mwisho wa onyesho lao walionekana kutumia nguvu hali iliyopelekea jukwaa la wasanii kutikisika na kutishia
usalama wa wasanii wegine.
“Unajua hawa
wasanii wanatumia sana nguvu na wananguvu katika kuimba na kucheza hadi wamevunja jukwaa
“walisikika baadhi ya wadau wakisema
ambao walikua karibu na mwandishi wa habari hii.
Ihhashi ni
mwanamuziki ambaye ambaye alitokea
katika kijiji kidogo cha Kwabiyela
Kwazulu Natal nchini Afrika Kusini.
0 Comments