MTOTO WA KOFFI OLOMIDE KUTOA BURUDANI MKESHA WA UHURU WA TANZANIA THAI VILLAGE MASAKI


AHMED  Jan Olomide  (Katitaki ) akifafanua jambo mbele ya waandishi wa habari leo asubuhi hawapo pichani m kushoto ni msanii maarufu nchini  Steve Mengele  a.k.a Steve Nyerere na kulia ni msanii wa ngoma na muziki wa asili Costa Siboka wote watapamba usiku huo.

NA MWANDISHI WETU, DAR ES SALAAM:

MWANAMUZIKI Ahmed Jan Olomide ambaye ni mtoto wa mwanamuziki nguli kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Koffi Olomide amesema kwamba ataudhihirishia umma wa watanzania na nchi  za jirani kipaji alichorithi kutoka kwa baba yake Olomide.

Akizungumza  leo asubuhi  katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika Hugo, Kinondoni Jijini Dar es Salaam  Olomide alisema kwamba tayari amekamilisha albamu yake inayokwenda  kwa jina la 100% Tchachoo yenye nyimbo kadhaa ambayo ataitambulisha Desemba 8 kwenye ukumbi wa Thai Village Masaki  Dar es Salaam.

Olomide ambaye pia licha ya kuwa yeye ni mwanamuziki mchanga amesema atakuwa na matamasha mawili ambalo hili la kwanza atasindikizwa na bendi ya Skylight wanao tamba na kibao chao kipya kinachokwenda kwa jina la ‘Kariakoo’.

Baada ya tamasha hilo  la kwanza  , onyesho la pili amepanga kulifanya na bendi ya The African Stars Twanga Pepetafa.Akizungumza kama anafahamu muziki wa Tanzania alisema anafahamu na kwa sasa amesema kuwa muziki huo umekua huku yeye akijitayarisha kurekodi na wanamuziki wa hapa nchini ili kuleta ladha tofauti na kujitangaza katika soko la muziki duniani kwa ujumla.
.

Huku akibainisha kwa kusema kwamba akiulinganisha muziki wa DRC na wa wanamuziki wa Tanzania alisema kwamba kwa sasa uko juu na kuwataka wanamuziki kuipenda sanaa hiyo na nyimbo zao kabla hazijapendwa na wengine

Post a Comment

0 Comments