SHINDANO LA REDD'S MISS TANZANIA LIKO PALEPALE KUFANYIKA OKTOBA 11 MLIMANI CITY

 Mkurugenzi wa Kampuni ya Lino International Agency , Hashim Lundenga ambaye ndiye Mratibu wa shindano la fainali za Redd's Miss Tanzania akifafanua jambo katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika leo kwenye hoteli ya JB Belmont Jijini Dar es Salaam anayefuata ni Meneja wa Kinywaji cha Redd's Premium Cold Victoria Kimaro.

 Kutoka kushoto ni Meneja wa Kinywaji cha Redd's Premiun Victoria Kimaro anayefuata kulia ni Hashim Lundenga.

Warembo wa shindano la Redd's Miss Tanzania wakiwa katika picha ya pamoja na Matron wao Glad.

(PICHA ZOTE NA MPIGAPICHA WETU)

DAR ES SALAAM,

MSHINDI wa shindano la Redd’s Miss Tanzania 2014 ataondoka na kitita cha sh. Mil.18 imefahamika.

Hayo yalisemwa leo na Meneja wa Kinywaji cha Redd’s Premium Cold  ambao ndiyo wadhamini wakuu wa shindano hilo Victoria Kimaro katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika  kwenye ukumbi wa JB Belmont Jijini Jijini  Dar es Salaam.

Kimaro alisema kwamba huu ni mwaka wao wa mwisho wa udhamini katika shindano hilo hivyo  wameamua kumpa mshindi fedha taslimu Mil.8 pia Mil. 10 ambayo ilikua anunuliwe gari nayo atapata fedha taslimu ili kama ataamua kununua gari ama kuweza kujilipia ada ya shule ama kufanya biashara hiyo itategea maamuzi ya mshindi huyo.

Kimaro anazitaja zawadi za warembo wengine kuwa ni atakayeibuka kuwa mshindi wa pili atapata kitita cha Mil.6, mshindi wa tatu atapata  Mil.4.2 mshindi wan ne atapata  Mil 3.2 wakati mshindi wa tano atapata Mil.2.2.

Warembo watakaoshika nafasi ya  6 hadi 15 wote kila mmoja taondoka na kitita cha Mil.1.2 huku wengine kuanzia wa 16 hadi 30 watapata kifuta jasho cha sh.700,000 kila mmoja alisema Kimaro.

Aidha aliongeza kwa kusema kuwa  katika shindano hili burudani kubwa itatolewa na msanii Omary  Nyembo ‘Ommy Dimpoz’ na wapambe wake na mwanamuziki anayetamba hivi sasa Vanessa Mdee .

Kimaro amesema kwamba maandalizi ya shindano hilo yamekamilika huku ukumbi wa Mlimani City ukiwa katika hatua nzuri za maandalizi ikiwemo kutengeneza jukwaa la aina yake.

Aliongeza kwa kusema kuwa licha ya kuwa wao wanamaliza mkataba na Lino lakini mrembo atakayeshinda atapata stahili zote aikiwemo kupata posho za kazi mbalimbali za akijamii ambazo atakuwa akizifanya kabla ya kwenda kuiwakilisha nchi kwenye shindano la kumsaka mrembo wa dunia (Miss World).

Wakati huohuo Mkurugenzi wa Kampuni ya Lino International Agency  Limited ambao ndiyo waratibu wa shindano hilo Hashim Lundenga alisema kwamba tiketi zimeanza kuuzwa katika maduka ya vipodozi ya Shear Illusions, Mlimani City na Millenium Tower Makumbusho Jijini Dar es Salaam.

Pia sehemu zingine ambazo tiketi zinapatikana ni  Steers  iliyopo Posta  Mtaa wa Samora na Hoteli ya  JB Belmont, pamoja na Club 777 iliyopo Mikocheni.Kiingilio cha juu ni sh. 100,000 na siti za kawaida sh. 50,000 ambapo ni watu 1500 ndiyo watakaopata  siti za kuona shindano hilo ndani ya ukumbi wa Mlimani City hivyo mashabiki wameomba kuchangamkia kununua tiketi.

Lundenga anawataja wadhamini wa shindano hilo kuwa ni  Redd’s Original, Marie Stopes Tanzania, Uchumi Super Market, Star TV,Continental Digital Media Content,S&D Collection, JB Belmont Hotel,Kijiji Beach  Hotel na True Vision Production.

Jumla ya warembo 30 wanawania taji hilo ambalo linashikiliwa na Redd’s Miss Tanzania 2013 Happiness Watimanywa.

Post a Comment

0 Comments