RAIS KIKWETE AKUTANA NA RAIS WA MALAWI PROF. MUTHARIKA

 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Rais wa Malawi Profesa Peter Mutharika  aliyemtembelea kumjulia hali kwenye hoteli ya Ritz Carlton katika kitongoji cha George Town jijini Washington DC, Marekani, ambamo wote walikuwa wamefikia.  Rais Kikwete na Rais Mutrharika, ambao walikuwa miongoni mwa viongozi wa Afrika walioalikwa kuhudhuria  Mkutano wa Kwanza wa Wakuu wa Nchi za Bara la Afrika chini ya uenyekiti wa Rais Barack Obama wa Marekani, walifanya maongezi mafupi yasiyo rasmi, ambapo pamoja na mambo mengine walizungumzia kudumisha mahusiano mazuri na ya muda mrefu baina  ya nchi hizo mbili.

(PICHA ZOTE NA IKULU)



Rais wa Malawi Profesa Peter Mutharika akisalimiana na Mama Salma Kikwete alipomtembelea kumjulia hali Rais Kikwetev  kwenye hoteli ya Ritz Carlton katika kitongoji cha George Town jijini Washington DC, Marekani, ambamo wote walikuwa wamefikia.  Rais Kikwete na Rais Mutrharika, ambao walikuwa miongoni mwa viongozi wa Afrika walioalikwa kuhudhuria mkutano wa Kwanza Wa Wakuu wa nchi za  Bara la Afrika chini ya Uenyekiti wa Rais Barrack Obama  wa Marekani walifanya  walifanya maongezi mafupi yasiyo rasmi, ambapo pamoja na mambo mengine walizungumzia kudumisha mahusiano mazuri na ya muda mrefu baina ya nchi hizo mbili.  






Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Rais wa Malawi Profesa Peter Mutharika  wakimsikiliza Waziri wa mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe Bernard Membe   kwenye hoteli ya Ritz Carlton katika kitongoji cha George Town jijini Washington DC, Marekani, ambamo marais hao  walikuwa wamefikia.  Rais Kikwete na Rais Mutrharika, ambao walikuwa miongoni mwa viongozi wa Afrika walioalikwa kuhudhuria  Mkutano wa Kwanza wa Wakuu wa Nchi za Bara la Afrika chini ya uenyekiti wa Rais Barack Obama wa Marekani, walifanya maongezi mafupi yasiyo rasmi, ambapo pamoja na mambo mengine walizungumzia kudumisha mahusiano mazuri na ya muda mrefu baina ya nchi hizo mbili. 

Post a Comment

0 Comments