Wema
Isaac Sepetu (25) ameibua viulizo baada ya kuonekana akirandaranda na
pete ya ndoa kidoleni ikidaiwa kuwa amevalishwa na Nasibu Abdul ‘Diamond
Platnumz’ kwa siri kubwa,Baada
ya kuwepo kwa habari nyingi kuhusiana na ishu hiyo, Ijumaa Wikienda
liliingia mzigoni kusaka ukweli wa ishu hiyo na kujua mbivu na mbichi.
Kwa
mujibu wa rafiki wa karibu wa mkali huyo wa sinema za Kibongo, hata
mashosti zake hawajui kinachoendelea zaidi ya kuulizana wao kwa wao
kuhusu nini kinaendelea huku kukiwa na hisia kuwa huenda wawili hao
wamefunga ndoa ya siri.
ALISHAMVISHA YA UCHUMBA
Kuna
maelezo kwamba Diamond alifanya hivyo ili kuzuia mwanaume mwingine
kumvisha Wema pete ya ndoa kwani alishamvisha ya uchumba tangu mwaka
2011 kwenye Ukumbi wa New Maisha ulipo Masaki jijini Dar.
WEMA LAIVU
Wiki iliyopita jitihada za kumnasa Wema akiwa na pete ya uchumba zilizaa matunda ambapo mwanahabari wetu alimuweka ‘mtukati.
Wema
alipotakiwa kuanika ukweli juu ya pete hiyo, alikubali na kueleza kuwa
ameamua kufunguka kwa mwanahabari wetu baada ya kuwa kimya tangu
alipovishwa pete hiyo.
HAJAFUNGA NDOA LAKINI…
Wema
alisema si kweli kwamba amefunga ndoa ya siri ila Diamond alimvisha pete
hiyo kama urembo akijua kabisa kwamba yeye ni wife material (anafaa
kuwa mke).
“Sijafunga ndoa jamani. Hii pete alininunulia baby wangu Nasibu (Diamond) wakati tukiwa South Africa (Afrika Kusini).
WEMA AIONA PETE, YAMVUTIA
“Alininunulia
na kunivisha tulipokwenda kwenye Tuzo za MTV Africa (MAMA). Nakumbuka
tuliingia kwenye duka moja nikaiona hii pete ikanivutia sana,
nikamwambia Nasibu ndipo akaninunulia na kunivisha palepale.
“Cha kushangaza ni kwamba imewatatiza wengi na kuhisi ndoa tayari.
“Hii pete
ndogo niliinunua mwenyewe hapahapa Bongo na kuivaa kama urembo tu,
hakuna tofauti na hilo kuhusiana na hizi pete nilizovaa kidole husika,”
alisema Wema ambaye kidoleni kwake kunaonekana pete mbili, kubwa na
ndogo.
WEMA NI WIFE MATERIAL?
lipoulizwa
kwa nini Diamond aliamua kumvisha pete hiyo kabla ya ndoa, Wema
alifunguka: “(kicheko) hilo sina uhakika nalo but amegundua mimi ni wife
material hataki kunipoteza. Kanipa heshima anayostahili kupewa
mwanamke...”
AMSHUKURU MTABIRI
Wakati
huohuo, Wema amemshukuru mtabiri, Maalim Hassan Yahya ambaye mwanzoni
mwa mwaka huu alitabiri kuwa mastaa hao wataoana mwezi ujao (Agosti)
mwaka huu akiomba Mungu na iwe hivyo.
“Natamani hiyo ndoa na nasubiria hiyo siku ili utabiri utimie, ni jambo la heri jamani,” alisema Wema.
DIAMOND VIPI?
Alipotafutwa
Diamond ili afunguke kuhusiana na ishu hiyo, simu yake ya kiganjani
iliita bila kupokelewa. Wakati huohuo, mashabiki wa mastaa hao,
wamewashauri mama Wema na mama Diamond kuwa kitu kimoja ili kufanikisha
ndoa hiyo ya watoto wao.
NI PETE YA PILI YA NDOA!
Ukiacha
pete hiyo ya ndoa aliyovishwa na Diamond, Wema aliwahi kuvishwa pete
kama hiyo alipofunga ndoa na jamaa aitwaye Jumbe Yusuf Jumbe ambayo
haikudumu hata mwezi mmoja.KUTOKA KWA MHARIRI
Ijumaa Wikienda linawatakia kila la heri mastaa hao ili kufanikisha jambo hilo ambalo linaongeza heshima kwenye jamii.
0 Comments