Hafla ya kuikabidhi rasmi ufadhili huo timu hiyo, ilifanyika katika ikulu ya Rais Ijumaa ambapo wachezaji kumi na moja wa timu hiyo walikabidhiwa tiketi za ndege kwenda Brazil.
Kitendo
cha Rais bila shaka ni jambo la kutaka kuwatia motisha wachezaji wa
timu ya taifa ambao hivi karibuni waliicharaza Djibouti mabao mawili kwa
moja katika duru ya kwanza ya michuano ya kuwania kombe la taifa bingwa
Afrika baadaye mwakani.
Mmoja
wa wachezaji hao alifurahi sana na kusema kuwa hatua ya Rais Kenyatta
kwao imetimiza ndoto yao. Rais atagharamia tiketi za timu hiyo kutazama
michuano, malazi na usafiri ingawa haijulikani ni mechi zipi
watakazotazama.
Hatua
ya Rais Kenyatta imewashangaza watu wengi sana nchini Kenya kwa kuwa
timu ya taifa ya Kenya haikuwahi kufuzu kushiriki michuano hiyo, sasa
wengi wanahoji hatua yake itasaidia nini?
Soka ya Kenya imekuwa ikikumbwa na changamoto si haba, usimamizi duni na wachezaji kukosa motisha ya kufanya vyema kwa ajili ya usimamizi huo mbaya.
Soka ya Kenya imekuwa ikikumbwa na changamoto si haba, usimamizi duni na wachezaji kukosa motisha ya kufanya vyema kwa ajili ya usimamizi huo mbaya.
Kenyatta na mkewe mama wa kwanza wa taifa Margaret Kenyatta wamewafadhili vijana hao kwa kima cha dola elfu arobaini.
Akitoa
ufadhili huo Kenyatta amesema lengo lake hasa ni kuwapa matumaini na
motisha ya kuweza kuinua mchezo wa soka nchini Kenya.
Pia ni kama ishara ya kuthamini wachezaji hao ambao hivi karibuni walishinda kombe la Cecafa.
Pia ni kama ishara ya kuthamini wachezaji hao ambao hivi karibuni walishinda kombe la Cecafa.
Kenyatta
mwenyewe hatakwenda na kikosi hicho bali amewaasa vijana hao kuwa
mabalozi wema wa Kenya nchini Brazil. Ufadhili huu unakuja miezi sita
baada ya Kenyatta kukubali kumlipa mshahara wa kocha wa timu hiyo kwa
miakja miotano ijayo.
Kenya
haijawahi kufuzu kwa michuano ya kombe la dunia lakini ziara hii kwa
vijana wa Harambee Stars itawafungua macho huku wakiwa na azma ya kufuzu
kwa michuano ya taifa bingwa Afrika mwaka 2015 baada ya kufuzu kwa duru
ya pili na kujiandaa kuchuana na Lesotho tarehe 18 Julai.
BBC
BBC
0 Comments