Usiku wa taarabu asilia ‘Old is Gold’ kufanyika Regency Hotel Jumapili hii



Na Andrew Chale
WAPENZI wa nyimbo za zamani za taarabu asilia nchini Jumapili hii ya Aprili 6,  wanatarajiwa kupata burudani safi na ya aina yake  kutoka kundi la Spice Modern Taarab,  ndani ya ukumbi wa  Regency Park Hotel,m iliyopo  Mikocheni, jijini Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Fabak Fashions, Asia Idarous Khamsin, ambao ni miongoni mwa wadhamini wa onyesho hilo, kwa kushirikiana na Regency Hotel,  amewasihi wadau kujitokeza kwa wingi kuufurahia kukumbushiana enzi za muziki wa mwambao wa taarab.

Asia Idarous alisema onyesho hilo pia litakuwa ni la kila siku ya Jumapili katika ukumbi huo ndani ya hoteli hiyo ya Regency, eneo lenye mazingira safi na  upepo mwanana  huku kiingilio kikiwa cha kawaida cha sh 5,000.
“Kila Jumapili Spice Taarab watakuwa wakitoa burudani ya nyimbo za mwambao hasa zile zilizokuwa zikipendwa,  kuanzia saa 12 jioni hadi saa sita usiku,” alisema Asia Idarous.

Asia Idarous pia alizitaja baadhi ya nyimbo ambazo zimekuwa gumzo kipindi hicho ni pamoja na ‘Pendo kitu cha hiari’, ‘Dunia ina fisadi’, ‘Kasha’ na nyingine nyingi. Aidha aliongeza kuwa  Regency  Park itakuwa ni kiota cha burudani ya miziki hiyo ya zamani huku usiku huo ukiwa unajulikana kama ‘OLD IS GOLD’ na watu mbalimbali wakitarajiwa kukutana hapo na kubadilishana ya zamani

Kwa upande wa Wadhamini katika usiku huo wa taarabu asilia ni pamoja na Times FM, Regency Park Hotel na Fabak Fashions, Pia alitoa wito kwa wadau wengine watakao kuwa tayari kudhamini kujitokeza kuchangamkia fursa hiyo kwa kuwasiliana na namba .0784263363 au0713263363

Post a Comment

0 Comments