Afisa
Tawala wa Mradi wa Wazazi na Mwana (MnW) Bwana Mashauri Ndebile
akimuonyesha Mkuu wa Wilaya ya Nkasi Mhe. Iddi Kimanta shehena ya vifaa
vya msingi kwa ajili ya kutoa huduma za dharura kwa kina mama wajawazito
na watoto wachanga Mkoani Rukwa. Vifaa hivyo mbalimbali vyenye thamani
ya Tsh. Milioni 912 vimetolewa kwa Mikoa miwili ya Rukwa na Mwanza,
ambapo kwa Mkoa wa Rukwa Mhe.
Kimanta
amevipokea kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa huo Injinia Stella Manyanya.
Jumla ya Zahanati 172 zitapatiwa vifaa hivyo ambapo kwa Mkoa wa Rukwa ni
zahanati 114 kwa Halmashauri za Nkasi na Sumabwawanga Vijijini na
Mwanza ni zahanati 64. Vifaa hivyo vimetolewa kwa ushirikiano wa
mashirika ya Plan International, Jhpiego na Africare.
Dokta
Neema Mamboleo mshauri wa Mradi wa Wazazi na Mwana akimuonyesha Mkuu wa
Wilaya ya Nkasi Iddi Kimanta kitanda maalum kwa ajili ya kusaidia watoto
wachanga waliozaliwa kabla ya muda kutimia na kuwa na matatizo ikiwa ni
sehemu ya vifaa hivyo vilivyotolewa na mradi huo. Msaada huo ni sehemu
ya misaada mbalimbali ya mashirikia hayo Mkoani Rukwa ambapo hivi
karibuni walitoa msaada wa "Ambulance" mbili na kujenga vyumba vya
upasuaji kwa Halmashauri za Nkasi na Sumbawanga Vijijini.
Dokta
Neema Mamboleo mshauri wa Mradi wa Wazazi na Mwana akimuonyesha Mkuu wa
Wilaya ya Nkasi Iddi Kimanta kitanda maalum kwa ajili ya kusaidia
kinamama wajawazito wakati wa kujifungua.
Mkuu
wa Wilaya ya Nkasi Mhe. Iddi Hassan Kimanta kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa
Rukwa Injinia Stella Manyanya akimkabidhi Mkurugenzi wa Halmashauri ya
Wilaya ya Nkasi Ndugu Kimulika Galikunga orodha ya mgao wa vifaa
mbalimbali kwa ajili ya Halmashauri hiyo.
Wadau
na wafanyakazi wa Africare Mkoani Rukwa wakiwa katika hafla hiyo fupi ya
makabidhiano. Kulia ni Ndugu Gasper Materu Mratibu wa Africare Mkoa wa
Rukwa.
Baadhi ya washiriki wa hafla hiyo.
Picha ya pamoja.
(Picha na Hamza Temba - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa @rukwareview.blogspot.com)
0 Comments