Katibu
Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana jana, aliendelea na ziara yake katika
mkoa wa Rukwa, kwa kutembelea wananchiwalioko pembezoni mwa mkoa huo,
ambapo alifika hadi katika Kata ya Wampembe iliyopo zaidi ya kilometa
100 kutoka mji mdogo wa Namanyere wilaya ya Nkasi ilimo kata hiyo.
Katika safari iliyomchukua zaidi ya saa tisa, Kinana na msafara wake
alikumbana na changamoto kubwa ya ubovu wa barabara kutoka Namanyere
hadi kwenye vijiji vya kata hiyo kutona na magari kunasa mara kwa mara
kwenye tope na makorogoro kwa kuwa barabara haijapata kufanyiwa
matengenezo kwa muda mrefu.
Kufuatia kujionea changamoto hiyo, Kinana amewambia wananchi wa vijiji
vya Wampembe na Ntemba, kuwa ataishauri serikali kuifanya barabara hiyo
iwe chini ya Wakala wa Barabara Nchini (TANROADS) badala ya sasa ambapo
ipo chini ya Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga na hivyo kuwa vigumu
kupatikana fedha za kutosha kujenga barabara hiyo.
Pichani
Kinana akizungumza na wananchi katika kijiji cha Wampembe, jana,Aprili
Mosi, 2014. Na zinazoendelea ni picha zaidi za ziara hiyo na changamoto
hizo alizokumbana nazo kama zilizvyopigwa na Bashir Nkoromo aliyeko
kwenye ziara hiyo.
Kinana akizungumza katika mkutano wa hadhara aliofanya katika Kijiji cha Wampembe, wilayani Nkasi mkoani Rukwa
Wananchi wa Kijiji cha Wampembe wakijimwayamwaya kwenye mkutano wao na Kinana
Kinana
akikagua ujenzi wa Kituo Cha Afya cha Wampembe wilayani Nkasi mkoani
Rukwa. Pamoja naye ni Mgaga Mkuu wa Kituo hicho, Dk. Mwabulambo Gwamaka
akimpa maelezo.
Kinana
akikagua ujenzi wa Kituo Cha Afya cha Wampembe wilayani Nkasi mkoani
Rukwa. Nyuma yake ni Mgaga Mkuu wa Kituo hicho, Dk. Mwabulambo Gwamaka
Kinana
akiwafurahia vijana aliowakuta wakifanya kazi katika kijiji cha
Wampembe kilichopo kilometa 100 kutoka mji mdogo wa Namanyere wilayani
Nkasi. Vijana hao wanafanyakazi katika sekta ya afya na ujenzi
Kinana mama, baba na watoto wakimpokea kwa hamasa kubwa Kinana katika kijiji cha Wampembe
Kinana
akizungumza na wananchi saa mbili usiku, baada ya kuzuia msafara wake
eneo la kijiji cha Ntemba kaya ya Kate akitoka Kata ya Wampemba kwenda
Sumbawanga mjini
Wananchi
katika kijiji cha Ntemba Kata ya Kate wilayani Nkasi wakimsikiliza
Kinana, alipoamua kuzunguza nao baada ya kumzuia njiani akitoka Wapembe
kwenda Sumbawanga
CHANGAMOTO ZA BARABARA
Kinana
akishiriki kuweka mawe kuweza magari kupita, baada ya magari ya msafara
wake kunasa kwenye pori la akiba la Nkasi, wakati Kata ya Wampembe
Kinana
akishiriki kuweka mawe kuweza magari kupita, baada ya magari ya msafara
wake kunasa kwenye pori la akiba la Nkasi, wakati akitoka Kata ya
Wampembe
Kinana
(kulia) akitazama moja ya gari la msafara wake ambalo lilinasa porini
katika harakati za dereva kujaribu kukwepa eneo baya kwenye barabara
katika pori la akiba la Nkasi, wakati akienda Kata ya Wampembe
Gari
la polisi waliokuwa wakisindikiza msafara wa kinana likisukumwa baada
ya kukwama katika barabara ya kutoka Wampemba kwenda Namanyere wilayani
Nkasi
Kinana
akiwa na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Rukwa, Hypolitus Matete walipokuwa
wakitembea kwa miguu baada ya kushindwa kupita kwa magari katika eneo
korofi la barabara
MTI WA NGUVU ZA KIUME
Waandishi
wa habari kwenye msafara wa Kinana akishangaa mti ambao unakarinia
kuanguka kutokana na kumegwa vbanzi na watu wanaoamini kwa vibanzi
kutoka mti huo ni dawa ya nguvu za kiume. mti huo upo pembeni mwa
barabara ambako magari ya msafara wa Kinana yalinasa wakati wa kwenda na
kutoka kijiji cha Wampembe.
Jamaa akigema kibanzi kwenye mti huo.
0 Comments