Na Boniface Wambura Mgoyo
Jopo
wa wang’amuzi vipaji limetangaza majina ya wachezaji 36 waliopataikana
katika mchakato wa maboresho ya Taifa Stars ulioshirikisha mechi za
mikoa yote ya Tanzania Bara na Zanzibar.
Kaimu
Mkurugenzi wa Ufundi wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF),
Salum Madadi amesema jopo hilo liling’amua vipaji 143 katika mchakato,
lakini waliochukuliwa kwa sasa ni hao 36 tu.
Amewataja
wachezaji waliochaguliwa katika mchakato huo kwa upande wa makipa ni
Abdulaziz Khatib Haji (Mjini Magharibi), Abubakar Abbas Ibrahim (Tanga),
Benedicto Tinoko Mlekwa (Mara) na Mtindi Kheri Ali (Kaskazini Unguja).
Kwa
upande wa mabeki wa pembeni waliochaguliwa katika mchakato huo ambao
upo chini ya udhamini wa Kilimanjaro Premium Lager ni Edward Peter
Mayunga (Kaskazini Pemba), Hussein Moshi (Tabora), Omari Kindamba
(Temeke) na Shiraz Abdallah (Ilala).
Mabeki
wa kati ni Abbas Ali Haji (Kaskazini Unguja), Ancy Abdon (Kagera), Emma
Namwamba (Temeke), Hussein Juma Akilimali (Njombe), Joram Nasson
(Iringa), Kayombo Silvanus Henrico (Ilala), Miraji Maka
(Mwanza), Ramadhan Ame Ramadhan (Kusini Unguja) na Said Juma Ali (Mjini
Magharibi).
Viungo
wapo Abubakar Mohamed Ally (Kusini Unguja), Hashim Ramadhan Magoma
(Shinyanga), Juma Said Jega (Lindi), Mtenje Alban Juma (Tanga), Ryna
Mgonyike (Temeke) na Yusuf Mpilipili (Temeke).
Washambuliaji
ni Abdallah Kagumbwa (Temeke), Abrahman Othman Ally (Mjini Magharibi),
Athanas Fabian Bayagala (Mbeya), Athanas Mdamu (Mwanza), Ayubu Hashim
Lipati (Ilala), Chunga Said (Manyara), Mbwana Mshindo Mussa (Tanga),
Michael David Mlekwa (Lindi), Mohamed Seif Said (Kusini Pemba), Omar
Athuman Nyenje (Mtwara), Paul Michael Bundala (Ilala), Ramadhan
Kapalamoto (Kinondoni) na Roman Nyapunda (Temeke).
Amesema
wastani wa umri wa wachezaji hao ambao watafanyiwa vipimo vya afya
Machi 19 na 20 mwaka huu kabla ya kambini Machi 21 mwaka huu, Tukuyu
mkoani Mbeya ni miaka 21.
Timu
hiyo itakuwa chini ya Madadi akisaidiwa na makocha Hafidh Badru, Salum
Mayanga na Patrick Mwangata. Aprili 13 mwaka huu utafanyika mchujo ili
kupata wachezaji wa mwisho watakaoungana na wale wa Taifa Stars
watakaoingia kambini Aprili 22 mwaka huu.
Taifa
Stars inatarajiwa kucheza mechi ya kirafiki mapema mwezi Mei mwaka huu
ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya mechi za mchujo kuwania tiketi ya
kucheza Fainali za Afrika (AFCON) zitakazofanyika mwakani nchini
Morocco.
0 Comments