Na Mwandishi
Wetu.Mwanza.
Victoria
Prince Bar wameibuka mabingwa katika fainali za mashindano ya Safari Lager
Nyama Choma 2014 yaliyofanyiaka mswishoni mwa wiki katika Uwanja wa Furahisha
jijini Mwanza na hivyo kuzawadiwa fedha taslimu Shilingi milioni moja(1,000
000/=) na Kikombe.
Mshindi wa
pili katika fainali hizo ni Gemestone Bar ambao walizawadiwa fedha taslimu
shilingi laki nane (800,000/=), mshindi wa tatu ni SD Executive Bar ambao
walizawadiwa fedha taslimu Shilingi laki sita (600,000/=), mshindi wan nne ni
Shooters Pub ambao walizawadiwa fedha taslimu Shilingi laki nne (400,000/=) na
nafasi ya tano ilichukuliwa na Lunala Bara ambao walizawadiwa fedha taslimu
Shilingi laki mbili (200,000/=)
Akizungumza
na wakazi jiji la Mwanza waliohudhuria fainali hizo, Mkuu wa Wilaya ya Ilemela,
Bi. Amina Masenza aliwashukuru kampuni
ya bia Tanzania(TBL) kwa kuanzisha mashindano hayo yenye mvuto wa pekee na
yenye kutoa ajira na kukuza kipato kwa wachoma nyama na si hilo tu hawa
walianza kwa semina malumu ya mafunza hivyo Serikali inaamini wanazingatia
taratibu zote za afya kwa kuandaa nyama inyokidhi viwango kwa mlaji.
Pili
aliwapongeza baa tano zilizoingia fainali kwani wao ndio baa bora katika baa
zote zinazochoma nyama mkoani humo na aliwaomba waendelee kuilinda hadhi na
sifa hiyo waliyopewa katika jiji la Mwanza na mwisho aliwapongeza mabingwa wa Victoria
Prince kwa kutwaa ubingwa wa mashindano ya Safari Nyama Choma kwa mwaka 2014 na
kuwaomba ambao hawakufanikiwa kupata nafasi hiyo wajiandae kwa mashindano
yajayo ya Safari Nyama Choma 2015.
Nae Meneja
wa Bia ya Safari Lager, Oscar Shelukindo aliwapongeza mabingwa wa mwaka 2014, Victoria
Prince na pia aliwashukuru wote walioshiriki toka mchakato ulipoanza mpaka
kufikia kumpata bingwa lakini pia aliwashukuru wakazi wa Mwanza waliojitokeza
kwa wingi kuja kushuhudia nani anatwaa ubingwa mwaka huu.
Mwisho
shelukindo aliwaomba wakatumie vyema zawadi walizopata kwa kuboresha majiko yao
kwa mashndano yajayo ya 2015.
0 Comments