Shaaban Dede bado amlilia Meddy Kitendawili



http://1.bp.blogspot.com/-cjdjW0iyNN0/TxQtbAxX1CI/AAAAAAAAUvc/JCJOdofxANw/s1600/Shaaban+Dede%252C+Msondo.JPG
Add caption

MTUNZI na muimbaji mahiri nchini, Shaaban Dede, amesema anaendelea kumkumbuka na kumlilia aliyekuwa 'swahiba' wake mkubwa, marehemu Mohammed Mpakanjia 'Meddy Kitendawili' aliyefariki karibu miaka mitano iliyopita.
Dede akizungumza na MICHARAZO, alisema licha ya ukaribu aliokuwa nao na marehemu Mpakanjia, lakini kukwama kwake kufanikisha mipango ya kufyatua albamu binafsi ya nyimbo zake za zamani humfanya amkumbuke zaidi.
Mwanamuziki huyo anayeiimbia Msondo Ngoma na aliyewahi kufanya kazi na bendi kama Mlimani Park, OSS na Bima Lee, alisema albamu hiyo ambayo ingekuwa na nyimbo sita na zingetolewa kwa mfuatano wa Vol, ilikuwa ifadhiliwe na Mpakanjia mipango iliyokuwa imeanza kabla ya swahiba wake huyo kukumbwa na mauti.
"Japo imepita miaka mitano takriban mitano sasa, bado  namkumbuka na kumlilia Meddy Kitendawili kwa mengio aliyonitendea na kuutendea muziki wa Tanzania. Ukiacha uswahiba wetu, pia kila nionapo nimeshindwa kufanikisha mipango ya kutoa albamu binafsi ya nyimbo zangu za zamani zilizotunga na kuimba katika bendi nilizopitia miaka ya nyuma naumia zaidi,"  alisema.
Dede alisema, hata hivyo anaendelea kupigana ili kufanikisha jambo hilo, hasa akisaka mfadhili mwingine wa kumpiga tafu.
Meddy Mpakanjia, aliyekuwa mume wa Mtangazaji na Mbunge maarufu wa Vijana, Amina Chipupa, alifariki Sept 14, 2009 miezi kadhaa tangu mkewe huyo kufariki wakati akiwa kwenye harakati za mapambano dhidi ya biashara ya dawa za kulevy

Post a Comment

0 Comments