Shavers amwadhiri Norton
• Adondoshewa vitasa vizito na kulamba sakafu
BONDIA Earnie Shavers alikuwa akijulikana kama bondia mwenye ngmi
nzito kuwahi kutokea katika uzito wa juu, wenyewe wakielezea kwa lugha
yao wakimwita ‘The Hardest Heavyweight Puncher Ever’
Bila shaka na kwa uhakika ndivyo ilivyokuwa, alikuwa ni bondia mwenye
ngumi za hatari, mabondia waliogopwa wakati ule kwa ngumi nzito na
nguvu akina Joe Frazier, Georgr Forema na hata Muhammad Ali
walichemka kumpiga kwa KO japo walimshinda katika mapambano yao.
Earnie Shavers aliingia rasmi katika ngumi za kulipwa mwaka1969. Mbali
na mabondia niliowataja, pia alitwangana na Ron Lyle, Jerry Quarry,
Jimmy Ellis, Jimmy Young na George Chuvalo kuwataja wachache na hakika
alikuwa si bondia mwenye ngumi nzito tu bali pia bondia mwenye kipaji
katika ngumi za uzito wa juu.
Bila shaka bondia Ken Norton alikuwa akijulikana kwa umahiri wake hasa
baada kumvunja taya Ali na kumshinda kwa pointi, katika pambano la
kwanza na kwa hivyo pambano hilo lilikuwa ni la kukata na shoka na
mashabiki wengi walimpa nafasi kubwa Norton ya kushinda pambano hilo.
Pambano la Norton dhidi ya Shavers lilifanyika Machi 23, 1979 japo
lilikuwa ni pambano au wakati ambao mabondia hawa wote walikuwa
wakielekea ukingoni mwa taaluma yao.
Ken Norton alikuwa amepoteza mapambano yake mawili ya kuwania ubingwa
wa dunia alipanda ulingoni akiwa na rekodi ya mapambano 41 akipigwa
5 huku 33 akishinda kwa ‘knockouts’ (KO). Pambano lake la mwisho la
KO lilikuwa dhidi ya bondia Randy Stephens. Norton alikuwa amepigwa na
kupoteza taji, alipigwa na Larry Holmes.
Earnie Shavers alkiuwa bado shupavu hata hivyo, akionekana bado
mwenye nguvu na stamina . Alikuwa ameshinda mapambano yake matatu kwa
KO dhidi ya Harry Terrell, John Girowski na Harold Carter kabla ya
kupanda ulingoni.
Shavers alikuwa na rekodi ya mapambano 57 akipigwa 7 na kutoka sare 1
huku mapambano 54 akishinda kwa ‘knockouts’ na rekodi za mabondia hao
zilifanya pambano hilo kuwa gumzo kwa hakika.
1. Raundi ya kwanza:
1. Raundi ya kwanza:
Mabondia wanakutanishwa katikati, baada ya kutambulishwa na mtangazaji
ulingo yaani ‘ring announcer’ wanakutanishwa kaikati, wanasalimiana
kisha kila mmoja anarejea kwenye kona yake huru (neutral corner).
Kengele ya kwanza inalia, Shavers anaanza kwa kasi bila kupoteza muda
na kumfuata Norton na kumbana kwenye kamba za ulingo, Shavers
anasukuma makonde ambayo yanapanguliwa na Norton na katika harakati
hizo, Norton alirusha ngumi ya kushoto na kumpata Shavers kwenye shavu
na Shavers akajibu na ngumi ya kushoto aliyeungnisha na ‘uppercut’.
Ngumi hizo zilikuwa si mchezo, zilikuwa ni ngumi za nguvu na
zinaonekana mkumuumiza Norton. Shavers anaona hali hiyo ya Norton
kuelemewa mapema tu na ngumi zake, anamfuata kwa kasi na kusukuma
‘uppercut’ ningine ya nguvu na mwanamme Ken Norton hana namna, konde
lile linakuwa zito zaidi kwake na anashuka chini na ‘kulamba’ sakafu.
Mwamuzi wa pambano hilo anamuhesabia Norton lakini anapofia hesabu ya
sita, Norton ananyanyuka. Mwamuzi anamwamuru Norton apanguse glavu,
anafanya hivyo kisha anaruhusiwa kuendela a pambano.
Shavers hapotezi muda, anamfuata kwa kasi Norton ambaye bado
anaonekana kuwa katika maumivu ya ngumi, anamshushia ngumi ndoano ya
kulia ‘right uppercut,’ na Norton anakwenda tena chini kama gunia la
mchele mbovu.
Norton anasubiriwa kunyanyuka lakini hajiwezi kabisa na mwamuzi
anamaliza pambano, Earnie Shavers anakuwa mshindi kwa TKO ambayo
kiukweli inapaswa kuwa KO bor
a. Pambano hili linaingia kwenye rekodi
za mapambano bora ya KO.
Kwa upande wa Earnie Shavers pambano hilo lilikuwa ni kila kitu kwake,
alikuwa na faida na hasa nguvu zake katika makombora. Katika pambano
hilo Shavers alimshushia makombora kadhaa Norton ambaye muda wote
alikuwa akirudi nyuma na kujikinga.
Ikumbukwe kuwa Ken Norton hakuwa bondia wa kurudi nyuma hata kidogo,
lakini siku hiyo alikuwa katika shida kubwa, alikuwa amepambana na
bondia mwenye nguvu
za mapambano bora ya KO.
Kwa upande wa Earnie Shavers pambano hilo lilikuwa ni kila kitu kwake,
alikuwa na faida na hasa nguvu zake katika makombora. Katika pambano
hilo Shavers alimshushia makombora kadhaa Norton ambaye muda wote
alikuwa akirudi nyuma na kujikinga.
Ikumbukwe kuwa Ken Norton hakuwa bondia wa kurudi nyuma hata kidogo,
lakini siku hiyo alikuwa katika shida kubwa, alikuwa amepambana na
bondia mwenye nguvu
0 Comments