Mganga Mkuu wa Hospitali ya Mkoa wa Mtwara, Ligula, Dkt. Shaibu Maarifa (katikati) akizungumza na Timu ya Ukaguzi
wa Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango
ilimpotembelea Ofisini kwake. Kushoto ni viongozi wa Timu hiyo, Prof.
Longinus Rutasitara (Kushoto) na Bibi Florence Mwanri (Wapili kulia).
Mganga Mkuu wa Hospitali ya Mkoa wa Mtwara, Ligula, Dkt. Shaibu Maarifa akisisitiza jambo wakati wa Timu ya Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango ilimpotembelea Ofisini kwake.
Mganga
Mkuu wa Hospitali ya Mkoa wa Mtwara, Ligula, Dkt. Shaibu Maarifa
(Wapili kulia, aliyenyanyua mikono) akiwaonesha eneo litakapokuwepo
Hospitali mpya ya rufaa mkoani humo wakati wa Timu ya Ukaguzi
wa Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango ilipofika
kujionea maendeleo ya maandalizi ya awali ya ujenzi wa hospitali hiyo.
Mthamini
Mkuu wa Ardhi wa Mkoa wa Mtwara, Bw. Abdallah Komba (aliyeinama)
akiwaelekeza namna ya hospitali ya rufaa ya mkoa huo itakavyokuwa
wakati Timu ya Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango ilipotembelea mradi huo.
Mmoja
wa viongozi wa Timu Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya
Rais, Tume ya Mipango, Bibi Florence Mwanri (Kushoto) akizungumza wakati
timu yake ilipofanya ziara ya kujionea maendeleo ya maandalizi ya awali
ya ujenzi wa hospitali hiyo.
======= ======= =========
MTWARA KUJIVUNIA HOSPITALI YA RUFAA
Na Saidi Mkabakuli
Wakazi
wa mikoa ya kusini ikiwemo Mtwara, Lindi, na Ruvuma inatarajiwa kupata
hospitali ya kisasa ya rufaa itakayojengwa katika eneo la Mikindani, nje
kidogo ya mkoa wa Mtwara katika lengo la kuhakikisha kuwa ukuaji wa
uchumi unakuwa shirikishi na kuendelea kuboresha huduma za jamii hususan
na afya katika mikoa hiyo.
Hayo
yamesemwa na Mganga Mkuu wa Hospitali ya Mkoa wa Mtwara, Ligula, Dkt.
Shaibu Maarifa wakati akizungumza wakati wa mkutano wa pamoja na Timu ya
Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango
ilipofanya ziara ya ukaguzi wa maendeleo ya katika mkoa huo.
“Mradi
wa hospitali ya Rufaa ya Mtwara umelenga kutoa huduma za rufaa kwa
kanda ya kusini hususan mikoa ya Mtwara, Lindi, na Ruvuma, hospitali hii
itakapokamilika inategemewa kuchukua wagonjwa wa nje na ndani
watakaohudumiwa kwenye vitengo mbalimbali vinavyojitosheleza kwa vifaa
na wataalamu, “ alisema Dkt. Maarifa. Kwa
mujibu wa taarifa za awali mradi ulianza kutekelezwa katika mwaka wa
fedha 2012/13 kwa fedha za Serikali zinazotolewa kupitia ngazi ya wizara
ambapo mpaka sasa ujenzi wa uzio kuzunguka eneo hilo umekamilika.
Akizungumza
wakati wa ziara hiyo, mmoja wa viongozi wa timu ya ukaguzi wa miradi ya
maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Bibi Florence Mwanri
alisema kuwa serikali inatambua umuhimu wa suala la afya kwa wakazi wa
mikoa ya kusini, na akatoa wito kwa uongozi wa mkoa kuzingatia na
kusimamia matumizi sahihi ya fedha za serikali katika mradi huo.
“Madhumuni
ya mradi ni mazuri hivyo mkoa kupitia wizara kuweka msukumo kwa
kuhakikisha mradi unakamilika na kutelezwa kwani utachangia kuboresha
huduma za afya katika maeneo ya kusini na kupunguzia wananchi mzigo wa
gharama kwa kufuata hospitali zilizo mbali na mikoa yao,” alisema Bibi
Mwanri ambaye ni Naibu Katibu Mtendaji anayeshughulikia Huduma za Jamii
na Maendeleo ya Idadi ya Watu.
Kwa
mujibu wa Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano (2011/12 -
2015/16) eneo la afya ni kipaumbele cha nne cha mkakati kwa lengo la
kuongeza maendeleo ya rasilimali watu na ujuzi ambapo Mpango unahimiza
kuwekeza katika elimu hasa katika elimu ya juu na vyuo vya huduma za
afya na uongezaji ubora na upatikanaji wa huduma hizo katika kujenga
nguvu kazi itakayoleta maendeleo ya kiuchumi na kijamii nchini Tanzania.
Serikali
imeaandaa Mpango wa Maendeleo wa Miaka Mitano ukiwa na lengo la kuwa na
mfumo madhubuti wa kutekeleza Dira ya Taifa ya Maendeleo 2025. Lengo la
Dira ni kuibadili Tanzania kuwa nchi ya uchumi wa kati ifikapo mwaka
2025.
0 Comments