Mbunge
wa Jimbo la Kitope Balozi Seif Ali Iddi akikagua Jengo jipya la Tawi la
Chama cha Mapinduzi la Kazole kabla ya kukabidhi vifaa kwa ajili ya
hatua ya ukamilishaji wa Linta.
Balozi
Seif Akimkabidhi Vifaa mbali mbali vya ujenzi Mwenyekiti wa CCM Tawi
la Kazole Nd. Sharif Makame Kundi ili kukamilisha hatua za linta.
Balozi
Seif ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa akimkabidhi fedha
Taslim Mwenyekiti wa Tawi la CCM Kazote Nd. Sharif Makame Kundi kwa
ajili ya fundi wa ujenzi wa Tawi hilo katika hatua ya Linta.
Balozi Seif akizungumza na Wanachama wa CCM Tawi la Kazole mara nbaada ya kukabidhi vifaa vya ujenzi kwa ajili ya Tawi hilo. Picha na Hassan Issa wa – OMPR – ZNZ.
********************************************
Zaidi
ya asilimia 95% imefikiwa katika ujenzi wa Matawi ya Kisasa ya Chama
cha Mapinduzi ndani ya Jimbo la Kitope liliomo katika Wilaya ya
Kaskazini “B” Mkoa wa Kaskazini Unguja.
Hali
hiyo imekuja kufuatia hatua za ukamilishaji wa Linta katika Tawi la
Chama cha Mapinduzi la Kazole likiwa miongoni mwa Matawi 19 ya Kisasa
yaliyo kwishajengwa kati ya Matawi 20 yaliyomo ndani ya Jimbo hilo.
Katika
kuunga mkono harakati za Wanachama wa chama cha Mapinduzi wa Tawi la
Kazole za ukamilishaji wa ujenzi wa Tawi lao Mjumbe wa Kamati Kuu ya
Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM Balozi Seif Ali Iddi alikabidhi vifaa
mbali mbali kwa ajili ya ukamilishaji wa linta na baadaye kujiandaa kwa
uwezekaji.
Balozi
Seif ambae pia ni Mbunge wa Jimbo la Kitope na Makamu wa Pili wa Rais
wa Zanzibar aliwaomba wanachama hao wa Tawi la CCM Kazole wajitahidi
kukamilisha kazi hiyo ili wao pamoja na Uongozi wa Jimbo hilo ujizatiti
katika hatua ya uwezekaji.
“
Ukweli nimefarajika sana kuona kwamba ile kiu yangu ya muda mrefu ya
kuona Matawi yetu 20 yaliyomo ndani ya jimbo letu yanakamilika kujengwa
katika mfumo wa kisasa kabla ya mwaka 2015 “. Alifafanua Balozi Seif.
Alisema
Chama cha Mapinduzi wakati wote kimekuwa kikisisitiza wanachama wake
Nchini kote kuendelea kujenga Ofisi za kisasa zenye hadhi ya Chama chao
zikienda sambamba pia na uanzishwaji wa miradi ya kiuchumi kwenye Ofisi
hizo.
Balozi
Seif aliwatahadharisha wanachama hao wa Chama cha Mapinduzi kujiepusha
na tabia za fitna ambazo zikiendekezwa zinaweza kusababisha mpasuko
miongoni mwa wanachama wenyewe kitendo ambacho kinaweza kupunguza nguvu
za chama hicho kikongwe Nchini.
Mjumbe
huyo wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM alielezea
matumaini yake kwamba juhudi za ziada zitachukuliwa ili kuona Tawi la
CCM la Kijiji cha Boma lililobakiika kati ya Matawi 20 yaliyomo kwenye
Jimbo hilo nalo linakamilika kujengwa.
Mbunge
huyo wa Jimbo la KitopeBalozi Seif alikabidhi vifaa vya ujenzi
kukamilisha hatua ya linta ya Tawi hilo la Kazote ambavyo ni pamoja na
Nondo,Matofali, Saruji na Kokoto.
Pia
alikabidhi Shilingi Laki 200,000/- za Fundi pamoja na Fedha taslimu kwa
Kikundi cha Ushirika cha kuweka na kukopa vyote hivyo vikiwa na thamani
ya Shilingi Milioni 1,700,000/-.
0 Comments