Afisa Mahusiano wa Airtel Tanzania, Jane Matinde (wa pili
kushoto) akizungumzia umuhimu wa promosheni ya Mimi ni Bingwa muda mfupi baada
ya kukabidhi shilingi milioni moja kwa baadhi ya washindi wa promosheni hiyo
(waliopo pichani). Kushoto ni Bw. Ramdhani Wefa, Kulia ni Philemon Nathaniel Mgaya
akifuatiwa na Bw. Msemwa Makuzi ambaye pia ni mshindi wa tiketi na wote wakiwa
wanatokea Dar es salaam.
######################################
Wakati
Kampuni ya mitandao ya simu za mkononi ya Airtel ikisubiria kuchezesha droo
kubwa ya shilingi Milioni 50 kupitia promosheni ya Mimi ni Bingwa, baadhi ya
washindi waliokwishapatikana wamejitokeza wakiisifia kampuni hiyo kwa kuratibu
promosheni zenye kulenga maendeleo kwa watanzania walio wengi nchini.
Washindi
hao wameainisha hayo muda mfupi baada ya kukabidhiwa pesa zao mapema wiki hii
kwenye ofisi za makao makuu ya Airtel ziilizopo Morocco jijini Dar es salaam.
Washindi
hao wamedai kuwa mara nyingi watu huwa hawaamini promosheni zinazoendeshwa na
kampuni ya simu kama Airtel na hivyo kujikuta wakibaki nyuma kwa kuogopa
kuthubutu.
“Mi
binafsi sikuwahi kumuambia mke wangu kwamba nashiriki kwenye promosheni ya Mimi
ni Bingwa sababu huwa akijua nashiriki ananikasirikia na kusema nina matumizi
mabaya ya pesa, lakini leo nimeibuka mshindi wa shilingi milioni moja yeye
akishuhudia na vilevile nimeshinda tiketi ya kwenda kushuhudia mechi ya
Manchester United kwenye uwanja wa Old Trafford,” alisema mshindi huyo Bw.
Msemwa Makuzi mkazi wa Dar es salaam.
Mshindi
huyo aliendelea kwa kusema, kwa hali ya kawaida ilikuwa ni ngumu kuamini kwamba
ameshinda shilingi milioni Moja na tiketi ya kwenda nchini Uingereza kushuhudia
mechi ya Manchester United kwenye uwanja wa Old Trafford.
“Kweli
mimi kama mtu mwingine yeyote wa kawaida iliniwia vigumu kuamini kwamba
nimeibuka mshindi wa pesa hizo na tiketi. Na imenichukua muda kuamini mpaka
sasa baada ya kukabidhiwa hizi milioni moja ndo naamini kweli mimi ni mshindi,”
alimalizia Bw. Makuzi.
Aidha
washindi wengine wamewaasa wananchi kote nchini kujitokeza kwa wingi katika
promosheni hiyo kwani ina manufaa makubwa kwa maendeleo ya mtu binafsi na taifa
zima.
“Kwa
kweli mi nawaambia watanzania wenzangu wasidhani hivi vitu ni masihara, watu
wanashinda kweli na maisha yao yanabadilika kupitia hizi pesa tunazopewa. Mimi
hapa naiwinda hiyo milioni 50 kwani nina uhakika nikishinda nitakuwa nimesahau
kabisa umasikini,” alisema Ramadhani Wefa ambaye ni mshindi wa milioni moja
kutoka Kinondoni jijini Dar es salaam.
Kwa
upande wake Afisa Uhusiano wa Airtel Tanzania, Jane Matinde alisema bado Airtel
inatambua na itaendelea kutambua umuhimu wa wateja wake hivyo haina budi
kuhakikisha inatoa huduma bora na zenye manufaa kwa wananchi wote kiujumla.
“Airtel
inaelewa fika kuwa wateja ndio kiini cha maendeleo ya kampuni hiyo na hivyo
inajitahidi kuhakikisha inatoa huduma bora za kuwanufaisha wateja wake na
kuleta maendeleo kwa taifa zima kiujumla,” alisema Jane.
0 Comments