MBOWE ASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI IRINGA,AACHIWA KWA KOSA LA KUZIDISHA MUDA KWENYE MKUTANO WAO WA HADHARA.



Pichani ni mwenyekiti wa CHADEMA,Mh. Freeman Mbowe akiwa sambamba na Mbunge wa jimbo la Kawe,Halima  Mdee wakiwa wameachiwa na jeshi la polisi akisindikizwa kwenda kupanda chopa katika viwanja vya mwembetogwa mara baada ya kudaiwa kuzidisha muda kwenye mkutano wao wa hadhara mkoani Iringa. (picha zote na denis mlowe)
 
MBOWE ASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI IRINGA.

Na Denis Mlowe,Iringa

MWENYEKITI wa Chadema Freeman Mbowe na Mbunge wa jimbo la Hai na Mbunge wa Jimbo la Kawe Halima Mdee walishikiliwa na Jeshi la Polisi, Kituo Kikuu Iringa, kwa kosa linalosemekana  kuzidisha muda wa mkutano uliofanyika katika kijiji cha Mgama wilaya ya Kilolo Mkoani Iringa.

Kwa majibu wa Mbowe alisema jeshi la polisi walimshikilia kwa masaa mawili kwa mahojiano na mkuu wa kituo cha polisi na kisha kumwachia huru.
Akizungumza na wafuasi wa Chadema kabla ya kupanda Helkopta na kuelekea mkoa wa Pwani akiambatana na Mbunge wa Kawe Halima Mdee aliwataka wananchama wa Chadema kuungana katika kukijenga chama bila hofu na kuwashukuru kwa kuwaunga mkono katika harakati za kuikomboa nchi.
Alisema wakati wanajiandaa kuondoka alipata malalamiko kutoka kwa kamanda wa Polisi wa Wilaya kuwa wamezidisha muda wa kufanya mkutano katika kijiji hicho.
Mbowe alisema kuwa chanzo kingine ni baadhi ya viongozi wa kijiji kuwadanganya wananchi katika mkutano uliotakiwa kufanyika katika vijiji vya kata ya Ukumbi kuwa watakuwepo  wabunge na mwenyekiti wa chama katika mkutano  kitu kilichosababisha kuwepo na dalili za ugomvi.


“Jeshi la polisi limetuhoji kuhusu mambo hayo na baada ya kuwaeleza walituachia huru na ila wamesema wakituhitaji watatuita lakini makamanda naomba sana mjenge chama na nawashukuru sana kwa kutuunga mkono katika harakati za kuikomboa nchi” Alisema Mbowe.

Post a Comment

0 Comments