MAYWEATHER ATAKA MASHABIKI WAKE WAMCHAGULIE BONDIA WA KUPIGANA NAE.



BINGWA wa dunia wa ngumi za uzito wa kati Floyd Mayweather amewataka mashabiki wake kuamua kama pambano lake litakalofuata liwe dhidi ya Amir Khan au Marcos Maidana. Khan ambaye ni raia wa Uingereza Desemba mwaka jana alisaini mkataba ambao unamuweka katika nafasi ya kupigana na Mayweather ambaye mpaka sasa hajawahi kupigwa na bondia yoyote. Khan mwenye umri wa miaka 27 ameshinda mapambano 28 kati ya 31 aliyopigana wakati Maidana ambaye ni raia wa Argentina yeye ameshinda mapambano 35 kati ya 38 aliyopigana.  Mayweather mwenye umri wa miaka 36 alituma ujumbe katika ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa twitter akiwataka mashabiki wake kumchagulia bondia wa kupigana naye katika pambano litakalofuata kati ya Khan au Maidana.Ni pigane na yupi kati ya Khan or Maidana??? Toa jibu kama wewe shabiki wake....
Justin Bieber na 50 Cent pamoja kwenye picha na Mayweather
TOP 10:
1) Floyd Mayweather
2) Manny Pacquiao
3) Andre Ward
4) Timothy Bradley
5) Wladimir Klitschko
6) Guillermo Rigondeaux
7) Adonis Stevenson
8) Sergio Martinez
9) Juan Manuel Marquez
10) Carl Froch

Post a Comment

0 Comments