Linah, Amin, Muumin, Mashujaa kuwasindikiza Extra Bongo




* Watazindua albamu yao ya Mtenda Akitendewa
* Choki kubatizwa jina gani Dar Live?
* Super Nyamwela, Banza waapa kufanya kufuru Jumamosi

Ally Choki (wa pili kulia) akizungumza na wanahabari mapema leo juu ya uzinduzi wa albamu yao siku ya Jumamosi. Wengine pichani toka kushoto ni Banzastone, Super Nyamwela na msemaji wa bendi ya Extra Bongo, Juma Kasesa
Hapo chachaaa!
WASANII nyota wa muziki wa kizazi kipya nchini, Linah na Amin kutoka THT pamoja na muimbaji nyota wa muziki wa dansi Prince Muwinjuma Muumin ni baadhi ya watakaowasindikiza wanamuziki wa bendi ya  Extra Bongo 'Wana Kimbembe' katika uzinduzi wa albamu yao ya ya pili iitwayo 'Mtenda Akitendwa' utakaofanyika siku ya Jumamosi jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na wanahabari mapema leo, Mkurugenzi wa bendi hiyo Ally Choki alisema uzinduzi juo unaotarajiwa kunogeshwa na utambulisho wa wasanii wapya wawili walionyakuliwa na bendi hiyo toka African Stars 'Twanga Pepeta', mnenguaji Asha Sharapova na rapa na muimbaji Greyson Semsekwa utafanyika kwenye ukumbi wa Dar Live-Mbagala nje kidogo ya jiji utasindikizwa na wasanii kadhaa nyota.
Choki alisema ukiondoa nyota hao wa THT, wengine watakaowasindikiza katika onyesho hilo linalotarajiwa kuibua jina jipya la Choki baada ya yale ya 'Mzee wa Farasi' au 'Mzee wa Tingatinga' kudumu kwa muda mrefu ni pamoja na pamoja na Malkia wa Mipasho nchini Hal hanisa Khadija Omar Kopa, Prince Mwinjuma Muumin, bendi ya Mashujaa na kundi la Makhirikhiri la Tanzania.
"Kambi ya maandalizi ya onyesho letu la uzinduzi wa albamu yetu ya pili ya 'Mtenda Akitendewa' inaendelea vyema na kwa taarifa tu kila kitu kimekaa vyema kwa onyesho hilo la Jumamosi ambalo tutasindikizwa na wasanii mbalimbali kama akina Linah, Amin, Khadija Kopa, Mwinjuma Muumin na Makhirikhiri wa Tanzania," alisema Choki.
Aliongeza kuwa siku ya uzinduzi huo tutawatambulisha wasanii wao wapya pamoja na kutambulisha mtindo mpya wa bendi hiyo wa 'Kimbembe'.
Awali Extra Bongo ilikuwa ikitamba na mtindo wa Kizigo na mwaka huu mpya wameingia na staili mpya ya 'Kimbembe' ambao ulitambulihswa kwa wanahabari katika shoo fupi ya kuonyesha maandalizi ya bendi hiyo yanavyozidi kunoga chini ya udhamini wa Global Publishers.
Mkurugenzi huyo ambaye ni mtunzi na muimbaji wa bendi hiyo alisema siku ya uzinduzi wataachia kwa pamoja audio na video ya albamu hiyo ya pili ya bendi hiyo baada ya ile ya 'Mjini Mipango', na kuonheza kuwa, audio itakuwa na nyimbo saba ikiwemo bonasi ya shoo ya sebene na video itakuwa na nyimbo sita tu.
Alizitaja nyimbo hizo za albamu hiyo ni 'Mtenda Akitendewa', iliyobeba jina 'Mama Shuu', 'Neema', 'Falsafa', 'Fisadi wa Mapenzi' na 'Bakutuka'.
Naye mwealimu na kiongozi wa safu ya uenguaji ya bendi hiyo, Mussa Hassan 'Super Nyamwela' alisema kuwa inafahamika wazi kuwa kwa Tanzania hakuna shoo kali na matata kama ya Extra Bongo hivyo asingependa kusema maneno mengi zaidi ya kuwataka mashabiki kujitokeza kwa wingi kupata burudani Dar Live ambapo alisema watafanya 'kufuru' kwa namna walivyopania kuendelea kufika nchini.
"Hili halina ubishi sisi ndiyp funika bovu nchini katika safu za uenguaji hivyo wapenzi wetu waje wapata kile ambacho hawajawahiu kukishuhudia kwani tumewaandalia mambo mapya kabisa," alisema Nyamwela.
Ramadhani Masanja 'Banzastone' kwa upande wake alisema Extra Bongo wanajua kazi zao na wanajua kitu gani mashabiki na wapenzi wa muziki wanataka na hivyo kusema Jumamosi itakuwa haitoshi kwa namna watakavyofunika mbaya.
"Waje wapate uhondo kwani tumejipanga mbaya, Extra Bongo hawana mpinzani na tumepania kuendelea kukimbiza mwanzo mwisho," alisema Banza.

Post a Comment

0 Comments