Mlezi
wa tawi la Yanga la Green Stone lililoko Mwananyamala , Yusuf Mwandeni
akimkabidhi kadi mwanachama mpya wa tawi hilo, Michael Machellah wakati
wa hafla fupi ya kukabidhi kadi kwa wanachama wapya iliyofanyika katika
Ukumbi wa CCM Mwinjuma Dar es Salaam.
Mwanachama
mpya wa Yanga, Michael Machellah akifurahia kadi yake ya uanachama wa
Klabu ya Yanga mara baada ya kukabidhiwa na mlezi wa tawi hilo, Yusuf
Mwandeni (wa tatu kushoto) wakati wa hafla fupi ya tawi hilo
iliyofanyika katika Ukumi wa CCM Mwinjuma Dar es Salaam.
Baadhi
ya Wanachama wa Yanga,tawi la Green Stone la Mwananyamala wakiwa katika
hafla fupi ya kukabidhi kadi kwa wanachama wapya iliyofanyika katika
ukumbi wa CCM Mwinjuma Mwananyamala Dar es Salaam.
Na Michael Machellah
TAWI
la Yanga la Green Stoni lenye makazi yake Mwananyamala CCM Mwinjuma
jana limekabidhi kadi tisa kwa wanachama wake wapya ikiwa ni sehemu ya
maandalizi ya uchaguzi wa viongozi wa tawi hilo.
Akizungumza
na waandishi wa habari mlezi wa tawi hilo la Green Stone mara baada ya
kukabidhi kadi hizo, Yusuf Mwandeni alisema tawi hilo mpaka sasa lina
jumla ya wanachama hai na wenye kadi 45 tangu lianzishe mwaka 20012.
Mwandeni
alisema tawi hilo kwa sasa liko katika harakati ya kuhamasisha wapenzi
na mashabiki wa timu ya Yanga wachukue kadi na waichangie Klabu yao kwa
kupitia kadi za uanachama na njia nyinginezo.
Tawi
la Green Stone linatarajia kufanya uchaguzi wiki ijayo Februari 2,2014
katika ukumbi wa CCM Mwinjuma kwa nafasi ya
Mwenyekiti,Katibu,Mwekahazina,Msemaji wa tawi na wajumbe wa kamati kuu
ya Tawi.
Nae
Mwenyekiti wa Tawi hilo, Lumole Matovolwa aliushukuru uongozi wa Yanga
kwa timu kuipereka Uturuki na juzi imeonyesha mambo mazuri ambayo
wameyapata huko baada ya kushinda mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom dhidi ya
Ashanti United lakini pia aliitakia timu maandalizi mema na mazuri kwa
yote wanayokabiliana nayo hivi karibuni tawi la Green Stone liko nyuma
yao kwa sapoti ya namna yoyote.
0 Comments