Naibu
Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Lazaro Nyalandu Serikali ameagiza kumalizwa
kwa migogoro ya mipaka baina ya Hifadhi ya Tarangire, Pori la Akiba la
Mkungunero na wananchi iliyodumu kwa muda wa takribani miaka kumi hadi
sasa.
Nyalandu amewataka wananchi wa vijiji vinavyopakana na hifadhi hizo
kuacha kuvamia maeneo yaliyotengwa kisheria kwani kwa kufanya hivyo ni kuleta
migogoro isiyo ya lazima.
Mhe.
Nyalandu alikuwa akiongea katika kikao maalum cha Kamati za Ulinzi na Usalama
za mikoa ya Manayara na Dodoma wilayani Babati mkoani Manyara zilizokutana kwa
ajili ya kujadili suluhu ya migogoro hiyo.
Aliongeza
kusema kuwa serikali imedhamiria kumaliza mgogoro hiyo kwa kuishirikisha jamii
kwa upana zaidi huku akisisitiza kwamba Serikali itaendelea kusimamia na
kutekeleza Sheria ya Uhifadhi bila kumuonea mwananchi yoyote na kwa kuzingatia
haki za binadamu.
|
0 Comments