MKUU wa mkoa wa
Iringa Dr Christine Ishengoma
ameanza kutembeza bakuri kwa
ajili ya kuichangia timu
ya Lipuli Fc inayohitaji kiasi cha zaidi ya
Tsh milioni 28 ili kufanikisha
timu hiyo kuendelea na
ligi daraja la kwanza hatua ya pili.
Huku akiwabana viongozi
wa timu ya
Lipuli Fc kuanza kueleza akiba ya fedha
ambayo wanayo hadi hivi sasa kabla ya
kuanza kuchangia wadau na
kuwataka kuwa na mikakati endelevu
ya kuweka akiba ya pesa.
Wakichangia
katika kikao hicho wadau
wa soka walitaka viongozi wa
timu ya Lipuli Fc kuonyesha umakini katika kuichangia timu
hiyo kwa kueleza mapato na
matumizi ya fedha
na kuwa na utaratibu mzuri
wa kuichangia timu hiyo.
Katibu wa timu
hiyo Wilye Chikweo alisema kuwa
usajili wa timu hiyo
utatumia kiasi cha Tsh
milioni 4 wakati kambi
ya timu itatumia Tsh milioni 10 pia mipira
20 kwa kila mpira
Tsh 50,000 pamoja na mahitaji
mengine yakiwemo ya marekebisho
ya uwanja Tsh 200,000
Hata hivyo alisema
kuwa hadi sasa
timu hiyo ina akaunti namba 01J207225200 Lipuli Football club benki
ya CRDB .
Kwa upande wake
mwenyekiti wa chama cha mpira
wa miguu mkoa wa Iringa Eliud
Mvella Wamahanji alisema kuwa klabu
hiyo ya Lipuli Fc kuwa ina tatizo kubwa .
Alisema kuwa ni kweli
utaratibu wa Lipuli Fc katika
kuendesha timu hiyo haujatumika vema .
Wamahanji alisema kuwa
timu hiyo inahitaji kucheza na
kusafiri ila bado timu
hiyo imekuwa ikiendeshwa kiugumu
ugumu kutokana na kukosa fedha.
“pamoja na mapungufu
ambayo timu inayo bado
viongozi hao wa Lipuli FC
imekuwa ikijitahidi kuendesha
timu hiyo na kweli ninawaoba
sana kuichangia timu
ya Lipuli Fc ili
kuweza kusonga mbele
zaidi mfano CRDB wanaweza
kusema watachangia milioni 15 na wengine
wakachangia milioni japo 10
kwa kila mmoja”
Kwa upande wake
mlezi wa timu
hiyo mkuu wa mkoa
wa Iringa Dr Ishengoma alisema
kuwa hadi sasa tayari amefanikisha
timu mbali mbali kusonga mbele
katika mikoa ambayo amepata kufanya kazi ukiwemo mkoa wa Ruvuma na Pwani na kuwa
hadi sasa bado mkoa wa
Iringa.
Hata hivyo aliwataka
wadau wa maendeleo katika mkoa
wa Iringa kujitokeza
kuichangia timu hiyo ya
Lipuli Fc kama sehemu ya kufanikisha
kuutangaza mkoa wa Iringa kama ulivyo mkoa
wa Mbeya na mikoa mingine ambayo imefanikiwa kimichezo.
Pia aliwataka wanaotaka
kuisaidia timu hiyo ya
Lipuli Fc kuingiza michango yao
katika akaunti ya timu iliyopo CRDB akaunti
namba 01J207225200 Lipuli Football club.
|
0 Comments