Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Joseph Warioba, akimkabidhi Rais Jakaya Kikwete, rasimu ya mwisho ya Katiba mpya, Dar es Salaam leo baada ya kumaliza kazi ya kukusanya maoni ya wananchi. Picha ya chini:Warioba akimkabidhi Rasimu ya Katiba, Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein.
Rais Jakaya Kikwete akiwakabidhi Rasimu ya Katiba Spika wa Baraza la
Wawakilishi Zanzibar, Pandu Ameir Kificho (kulia), Rais mstaafu wa Awamu
ya Pili, Ali Hassan Mwinyi (katikati) na Waziri Mkuu wa zamani, Cleopa
Msuya (kushoto) baada ya kukabidhiwa rasmi na Mwenyekiti wa Tume ya
Mabadiliko ya Katiba, Jaji mstaafu Joseph Warioba, Dar es Salaam
Rais Jakaya Kikwete (kulia), akimkabidhi Rasimu ya Katiba Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad.
Baadhi ya viongozi wa vyama wakiwa katika hafla hiyo.
Viongozi wastaafu na waasisi wa Tanzania, wakiwa wameshikilia rasimu
hiyo, baada ya kukabidhiwa na Rais Jakaya Kikwete jana. Kutoka kushoto
ni Balozi mstaafu Job Lusinde, Sir George Kahama, Hassan Nassor Moyo na
Jaji mstaafu, Mark Bomani na aliyekuwa Mkuu wa Majeshi, Mirisho
Sarakikya
Baadhi ya wananchi na wanazuoni wakiwa katika hafla hiyo ya kukabidhiwa
Rais Jakaya Kikwete na Dk. Ali Mohamed Shein, rasimu ya mwisho ya
katiba.
0 Comments