LOWASSA NA MAKAMBA , HIZI FEDHA MNAZOGAWA MNAZITOA WAPI?




-Siyo siri kwamba wasaka urais wawili wakubwa ndani ya CCM, January Makamba na Edward Lowassa, wamekuwa wakizunguka nchi wakigawa mamillioni ya fedha kwa wananchi ili waungwe mkono katika mbio zao za urais 2015

-Siyo siri kwamba Bw. Makamba Jr. Alikuwa mtumishi wa umma wa kawaida, lakini baada ya muda mfupi, huyu kijana amatokea kuwa na ukwasi mkubwa wa kifedha kiasi kwamba anadhamini vijana, na makundi mengi huku akigawa rushwa za waziwazi. Zanzibar aligawa simu aina za Samsung Galaxy S3 ambazo zinagharimu zaidi ya Tsh 700,000 kwa zaidi ya vijana 200 wa UVCCM. Kwa mahesabu ya juu juu, thamani ya simu 200 ni million 140. Hizi fedha amezitoa wapi January Makamba?

Naye Waziri Mkuu Mstaafu  Lowassa licha ya kwamba jimboni kwake ni masikini wa kutupwa, amekuwa akizunguka nchi nzima akigawa mabillioni makanisani na kwenye misikiti. Hizi fedha naye kazitoa wapi? Hawa watu wanatafuta nini Ikulu? Kwa nini CCM inyamazie tabia za hawa watu? January akumbuke kwamba ubunge wake aliupata kwa hila baada ya babake Mzee Yusuf Makamba kumfanyia hila Mzee. Shelukindo.

Naitahadharisha chama changu CCM kwamba, ikiwa itafanya makosa ya kuwapitisha hawa watu wawili ambao wanazunguka nchi wakigawa rushwa hadharani bila vyombo vya dola kuwahoji, nitafanya maamuzi magumu ya kuongoza uasi ndani ya CCM ili tuwape wananchi njia mbadala ya uongozi, hata kama itamaanisha kuwaunga mkono viongozi safi wa upinzani. Hawa vinara wawili siyo tu wanakiuka miiko na maadili ndani ya CCM, kwa maana kwamba muda wa kampeni bado, kadhalika wanavunja sheria za nchi kwa kugawa rushwa.

January hajawahi kuchaguliwa kwenye cheo chochote kile hata ubunge, lakini badala ya kufuata njia halali, yeye anaendekeza rushwa huku akimpiga majungu waziri wake pale wizara ya Sayansi na Teknolojia. Natokea jimboni Bumbuli, lakini cha ajabu, Mzee Makamba na Mwanaye wanatangaza jimboni kwamba January Akiwa Rais Tanga itakuwa kama Singapore? Really? Tutafika kweli kwa mwendo huu? Hawa jamaa wanakimbilia ikulu kufata nini?

Post a Comment

0 Comments