MABONDIA
Said Mbelwa 'Moto wa Gesi' na Shabani Kaoneka 'BSS' watapima uzito
siku ya jumamosi ya tarehe 9 novemba utakaofanyika Amana CCM Ilala
kwa ajili ya mpambano wao wa jumapili ya tarehe 10 novemba mpambano
utakaofanyika katika ukumbi wa Zulu Paradais Pugu Kilumba, akizungumzia
mpambano huo mratibu ambaye pia ni kocha wa kimataifa wa mchezo wa
masumbwi nchini Rajabu Mhamla 'Super D' amesema kila kitu kimesha
kamilika kilichobaki ni kupima uzito siku ya jumamosi ambapo mabondia
hawo wanatakiwa wawe na KG 76 kila mmoja kwa ajili ya mpambano huo wenye
upinzani wa ali ya juu kutokana na kila mmoja kujigamba kuwa atamtwanga
mwenzie raundi za awali mabondia hawo waliokuwa wakitafutana kwa mda
mrefu sasa tunahesabu masaa macheche kwa ajili ya mpambano wao wa raundi
8 mbali na mbambano huo siku hiyo kutakuwa na mapambano mengine ya
utangulizi ambapo bondia Hamza Mchanjo atamenyana na Tony King wakati
Chirambo Hemed atafaana na Sharifu Mzezele nae Twalibu Mchanjo
atapambana na Mohamed Kashinde uku bondia Adamu Ngange atapambana na
Shabani Mtengela 'Zunga Boy' mbali na kuwepo kwa mapambano hayo siku
hiyo kutakuwa na uzinduzi wa DVD mpya za bondia Said Mbelwa ambapo
alipocheza nje ya nchi zikiwemo ujerumani, afriganstan pamoja na DVD za
ngumi kali mbazo zitakuwa zikiuzwa kwa ajili ya kuhamasisha mchezo wa
masumbwi nchini pia kutakuwa na vifaa mbalimbali vikiuzwa kwa bei nafuu
kwa wadau wa mchezo wa ngumi kama vile, clip bandeji,gum shit,bukta,
glove na vifaa mbalimbali vya masumbwi |
0 Comments