Diwani wa Kata ya Msongola, Ukonga, Dar
es Salaam, Angel Malembeka (kulia) ameipiga tafu timu ya soka ya Uhuru
FM, kwa kuipatia jozi mbili za jezi na mipira miwili ikiwa ni sehemu ya
kuimarisha ushirikiano baina ya timu hiyo na kata yake. Pichani, Diwani
huyo akikabidhi vifaa kwa uongozi wa timu hiyo, Angel Alikimali na
Furaha Luhende, katika hafla fupi iliyofanyika nje ya Jengo la CCM mkoa
wa Dar es Salaam, leo. Wakati Luhende ni Mwenyekiti wa timu hiyo,
Akilimali ambaye ni Kaimu Mkurugebzi Mtendaji wa Uhuru FM ni mlezi wa
timu hiyo.
Akilimali akimshukuru Masala Mabula
ambaye ni mchezaji aliyeibuliwa kipaji chake katika michuano ya
Malembeka Cup iliyomalizika hivi karibuni ambaye sasa anajiandaa kwenda
Msumbiji kucheza soka la kulipwa. Masala alifuatrana na Diwani huyo
(kulia)
Luhende na Akilimali wakifurahia vifaa hivyo baada ya kukabidhiwa na diwaniDiwani na Akilimali wakiwa na baadhi ya waandishi na watangazaji wa Uhuru baada ya makabidhiano hayo.
Mtangazaji wa Uhuru FM, Mhina Dungumalo akimhoji diwani huyo baada ya makabidhiano Imetayarishwa na theNkoromo Blog
0 Comments