HABARI zilizotufikia hivi punde mtandao huu,
zinasema kuwa, Baba Mzazi wa msanii wa Filam nchini na Miss Tanzania wa mwaka
2006, Wema Sepetu, Balozi Issac Abraham
Sepetu, amefariki Dunia asubuhi ya leo katika Hospitali ya TMJ Mikocheni
jijini Dar es Salaam, alikokuwa amelazwa.
Aidha imeelezwa kuwa, Balozi Sepetu alikuwa amelazwa
katika hospital ya TMJ akitibiwa ugonjwa wa Kisukari na kiharusi uliokuwa ukimsumbua.
Hadi umauti unamkuta,Balozi Isaac Sepetu alikuwa ni
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Uwekezaji wa Vitega Uchumi
Zanzibar.
Mtandao huu unaungana na waombolezaji wote wa Msiba
huu na Mwenyezi Mungu, Aiweke Roho ya Marehemu Balozi Isaac Abraham Sepetu,
Mahala Pema Peponi .
-Amen-
0 Comments