Mshindi wa taji la Talent Redds Miss Tanzania Clement aliyekaa katikati katika picha ya pamoja na warembo aliowashinda katika shindano hilo.(Picha na Francis Dande)
VITUO vya kuuza tiketi za Redds Miss Tanzania
vyatangazwa.
Hayo yalisema Jumamosi iliyopita Septemba 14 usiku na Mkuu wa Itifaki swa
shindano hilo pendwa katika shindano la kumsaka mrembo mwenye kipaji (Miss
Tanzania Talent Show 2013) lililorindima katika ufukwe wa hoteli ya Giraffe
View Mbezi Beach jijini Dar es Salam.
Akiwa juu ya jukwaa Makoye alisikika akitangaza maeneo
ambayo tiketi hizo zitapatikana ni pamoja na Maduka maarufu jijini Dar es
Salaam yanayouza vipodozi vya wanawake Shearillusion yaliyopo maneo ya Mlimani City, Millenium Tower na Mbezi.
Aidha maeneo
mengine ni pamoja na Faback Fashion
Mikocheni kwa Mwalimu Nyerere , Steers na Rose Garden.
Kiingilio
cha kwenda kumshuhudia mlimbwende wa mwaka huu ni sh.100,000 na 50,000.
Wakati
huohuo mrembo aliyekuwa amevalia namba
18 Prisca Clement kutoka Kanda
ya Kinondoni aliweza kuibuka mshindi wa shindano la Redds Talent Miss Tanzania
2013.
Kwa ushindi
huo Prisca moja kwa moja ameingia katika warembo 15 bora wa Redds Miss Tanzania
mwaka huu.
Prisca
aliweza kuonesha umahiri wa kucheza na muziki huku ukiwa na mahadhi ya kiafrika
sambamba na kucheza na moto akiula bila ya kungua jambo ambalo lilivitia watu
na kushangiwa kwa muda wote aliokuwa jukwaani.
Baadhi ya
warembo wengine waliopanda jukwaani lakini bahati haikuwa yao waliweza kucheza
katika miondoko mbalimbali ya muziki kama vile twist, miondoko ya Kanda
Bongoman,kihindi, yupo aliyejaribu kucheza kama mwanamuziki wa kufokafoka ,
yupo aliyeigiza kucheza na kuvaa kama Michael Jackson, Monica Seca na wengineo
wengi.
Shindano
hili litafanyika Septemba 21 kwenye ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam
ambapo msanii nyota na wakimataifa atapamba onesho hili pamoja na wasanii wa
hapa nyumbani.
Mwisho
Shindano la
Redds Miss Tanzania limeandaliwa na Kampuni ya Lino International Agency ikiwa
chini ya Mkurugenzi wake Hashim Lundenga
na kudhaminiwa na ,kinywaji cha Redds Original, Marie Stopes, IPP, Star
TV,Hoteli ya Giraffe View ambako warembo wamekuwa wakiweka kambi kwa mwaka wa
10 sasa.
0 Comments